"Viwanda" ndivyo viwe gharama ya maisha ya waTanzania? Hoja yako hapa inakushusha daraja. Kulalamikiwa uongozi/rais hakujawahi kufikia kiwango hiki na kwa mambo mengi mbalimbali kiasi hiki. Samia kashuka sana. Mbaya zaidi, badala ya kuelewa yanayo lalamikiwa, hotuba zake zinazidi kuchochea moto, akidhani kuvimba kwake ndiko kutatia watu hofu.
Ndiyo, Mmarekani anastahili kunyooshewa vidole kwa mengi yanayofanywa nje ya nchi hiyo; lakini hakuna kiongozi aliye thubutu kufanya ujinga ndani ya nchi hiyo akabaki salama kama hawa wa kwetu. Kwa hiyo, hawa wakikoromewa na huyo huyo Mmarekani, pamoja na ubaya wake unao julikana nje, raia wanaonyanyaswa na viongozi wao kama Samia ni lazima washangilie.
Kama umesoma Ukraine, halafu ukaandika yale uliyo andika kule mwanzo, inaonyesha hukujifunza vizuri uhusiano wao na Urusi/Marekani ulivyo geuka kuwa sasa hivi.