Wamiliki wa Feza Schools ni kikundi chenye muunganiko na Fethullah Gulen, Mturuki anayeishi uhamishoni Marekani ambaye anahusishwa na jaribio la mapinduzi mwaka 2016 lililofeli.
Fethullah Gulen ni Mwislamu mwenye wafuasi wengi nchini Uturuki. Wakati Recep Tayyip Erdogan anatafuta kuungwa mkono aliomba msaada wa Gulen ili waumini wamkubali. Erdogan hana mambo ya dini sana kama viongozi wa Uturuki walivyo siku zote hasa baba wao wa taifa Mustafa Kemal Atatürk. Ndio maana Uturuki haina mambo ya dini dini na unaona wanapigilia suti hawana mambo ya kanzu.
Erdogan alipata msaada wa Gulen ambaye tuseme ni mgombea wa Zanzibar aungwe mkono na Sheikh Ponda kwa sasa. Erdogan alipopata maana yake Gulen akawa na nguvu kifedha na kiutawala. Akaanzisha vyuo vingi na shule, akasambaza Islamic movement (ambayo ni agenda ya Uturuki kitaifa). Akawapa connection watu kibao jeshini, vyuoni maprofesa, vyombo vya habari, wafanyabishara, usalama wa taifa, etc.
Hao watu sasa hivi wanaitwa Gulenists na wamefutwa sana kazi zao baada ya lile jaribio la mapinduzi. Erdogan alikuwa serious kiasi alisamehe wafungwa ili apate nafasi ya kufunga washiriki waliokuwa wengi. Majaji walifutwa, watu wakafukuzwa kazi, wanajeshi zaidi ya 10,000 waliwekwa ndani kusubiri uchunguzi.
Mojawapo ya shule za movement ya Gulen ni Feza sasa. Mwanzo zilianza ni agenda ya serikali kuongeza influence geopolitically ila Gulen akawa mtu mkubwa sana. Yani tufanye Sheikh Ponda (angekuwa msomi sana) alivyo na influence kidini, bado umuongeze awape watu connection kila idara, nao wawape watu connection anakuwa mtu hatari zaidi. Gulen aligundua ni threat kwa Erdogan anakimbilia Marekani ambao inasemekana walijua wakati anapanga jaribio.
Huyu balozi anatetea serikali yake iliyomuajiri ila kuna haja ya kutopuuza sio kwa Feza bali kwa miradi yote ya "msaada" kutoka kwa mataifa yenye ajenda binafsi.