Balozi wa Uturuki: Shule za Feza zinaidanganya Tanzania, naamini Serikali itachukua hatua

Balozi wa Uturuki: Shule za Feza zinaidanganya Tanzania, naamini Serikali itachukua hatua

Alilolisema balozi hata Boss wake alimwambia Marehemu Magufuli Kama sikosei. Tambua hayo ni ya kwao huko sisi hayatuhusu madhali wanafuata sheria ya nchi wafungiwe ili iweje? Nitashangaa kama huyu balozi atasikilizwa na uongozi wa nchi yetu kwa Sasa maana Boss wake alitolewa nje kiaina na Hayati. Hiyo ya kuwa ni waturuki ndio umeisikia leo? Au hutaki waturuki kuwekeza Tanzania? Sijakuelewa
Uturuki haitaki shule zifungwe, inataka zitaifishwe au ziuzwe kwa wamiliki wengine
 
Hao ni wawekezaji wazuri tu wana shule nyingine inaitwa Shamsiye ipo Bunju ni miongoni mwa shule za feza schools.

Ugomvi wao wa ndani sisi hautuhusu kabisa. Sisi tunataka vijana wetu wapate elimu bora kutoka shule hizo.

Kitaifa mitihani ya form 4 shule mbili za feza boys na feza girls zimeingia top ten.

Pia wana feza international ambazo hazifuati mtaala wa kwetu bali mitaala ya kimataifa kama ilivyo International school of Tanganyika.
kwa stail hiyo hili vuguvugu kuisha sio leo kila mmoja ana sababu zake
 
Nyie wote mnamshambulia Balozi bila kujua alichosema balozi ....

Nasema siku mkijua / mkielewa alichosema Balozi itakuwa too late na hamtaweza kufanya chochote kama Taifa ... Poleni sana Watanzania wenzangu kwa kukosa maarifa ...
 
swali lingine la kujiuliza huu mgogoro serikali inaona ni sawa [emoji848][emoji848]
 
wajamaa siku wanaweza kupiga bomu pale na watoto wetu wakiwa darasani[emoji848][emoji848]
 
Mbona Habari za zamani sana ambazo zinarudishwa tu
Hakuna mapya ?
 
Ni kama vile Mbowr akafungue shule kenya af balozi wa tanzania nchini kenya alete figisu kwa shule hizo
Halafu ubalozi wa Tanzania huko Kenya utoe kibali cha hao wanafunzi wa huyo mpinzani kuja Tanzania kila mwaka. Najiuliza sipati jibu
 
Maana yake ni sisi tupime, kipi muhimu kati ya kuwa na hizi shule hapa TZ na kuwa na uhusiano mzuri na Uturuki.
Rais Edogan alivyonusurika kupinduliwa aliendesha oparesheni kali dhidi ya waasi na ikabainika hawa wenye shule ni wafadhili wa waasi. Anachotaka ni kukata mirija yao ya fedha
Anachotakiwa ajitathmini kwa nini alitaka kupinduliwa badala yake analipiza kisasi, na hii ni tabia ya viongozi wengi
 
Wamiliki wa Feza Schools ni kikundi chenye muunganiko na Fethullah Gulen, Mturuki anayeishi uhamishoni Marekani ambaye anahusishwa na jaribio la mapinduzi mwaka 2016 lililofeli.

Fethullah Gulen ni Mwislamu mwenye wafuasi wengi nchini Uturuki. Wakati Recep Tayyip Erdogan anatafuta kuungwa mkono aliomba msaada wa Gulen ili waumini wamkubali. Erdogan hana mambo ya dini sana kama viongozi wa Uturuki walivyo siku zote hasa baba wao wa taifa Mustafa Kemal Atatürk. Ndio maana Uturuki haina mambo ya dini dini na unaona wanapigilia suti hawana mambo ya kanzu.

Erdogan alipata msaada wa Gulen ambaye tuseme ni mgombea wa Zanzibar aungwe mkono na Sheikh Ponda kwa sasa. Erdogan alipopata maana yake Gulen akawa na nguvu kifedha na kiutawala. Akaanzisha vyuo vingi na shule, akasambaza Islamic movement (ambayo ni agenda ya Uturuki kitaifa). Akawapa connection watu kibao jeshini, vyuoni maprofesa, vyombo vya habari, wafanyabishara, usalama wa taifa, etc.

Hao watu sasa hivi wanaitwa Gulenists na wamefutwa sana kazi zao baada ya lile jaribio la mapinduzi. Erdogan alikuwa serious kiasi alisamehe wafungwa ili apate nafasi ya kufunga washiriki waliokuwa wengi. Majaji walifutwa, watu wakafukuzwa kazi, wanajeshi zaidi ya 10,000 waliwekwa ndani kusubiri uchunguzi.

Mojawapo ya shule za movement ya Gulen ni Feza sasa. Mwanzo zilianza ni agenda ya serikali kuongeza influence geopolitically ila Gulen akawa mtu mkubwa sana. Yani tufanye Sheikh Ponda (angekuwa msomi sana) alivyo na influence kidini, bado umuongeze awape watu connection kila idara, nao wawape watu connection anakuwa mtu hatari zaidi. Gulen aligundua ni threat kwa Erdogan anakimbilia Marekani ambao inasemekana walijua wakati anapanga jaribio.

Huyu balozi anatetea serikali yake iliyomuajiri ila kuna haja ya kutopuuza sio kwa Feza bali kwa miradi yote ya "msaada" kutoka kwa mataifa yenye ajenda binafsi.
Na yeye Sasa hivi anajitadi sana kwenye dini
 
kuna shida uturuki... tutajua tu... tuna fanyia kazi taarifa za balozi, tanzania sio mahal salama kwa magaidi
 
Back
Top Bottom