Balozi zetu toeni fursa kwa Wajasiriamali

Balozi zetu toeni fursa kwa Wajasiriamali

Valencia_UPV

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2016
Posts
6,974
Reaction score
8,750
Inashangaza Sana Balozi zetu huko ughaibuni hazitoi taarifa za fursa zilizopo huko. Fikiria nchi za Middle and Far East zilivyo na fursa ya Ajira, chakula na Ujenzi Ila wenzetu ubalozini wametulia tu. Qatar World Cup 2022 inakuja Ila utakuta hawa ndugu zetu hawana huo muda. Why?

NB: Ubalozi wetu Pretoria pasua kichwa Kwa wanaotaka kuja kutalii nchini. Unawashauri wageni waende Dubai.


opportunities-restaurant-business-uae-578x289.jpg


images - 2022-03-27T084109.923.jpeg

Screenshot_2023-04-11-20-36-09-20_3d9111e2d3171bf4882369f490c087b4.jpg


==
Soma Mchango wa Balozi za Tanzania kwenye kusaidia upatikanaji wa Ajira kwa Watanzania
 
Hivi vyeo wanapewa makada badala ya watu wenye uwezo
Nimefika Qatar wamejaa watu kutoka Afrika hususani Kenya, Uganda, Ghana na Nigeria. Ukiwauliza wanasema taarifa waluzipata kupitia Balozi hapa Doha. Baadhi ya kampuni toka kwao zikaomba tenda zikapata ndo wakaleta watu wao. Sisi Sasa!ukifika hapo ubalozin ukaongea Kiswahili tu wananuna.
 
Nimefika Qatar wamejaa watu kutoka Afrika hususani Kenya, Uganda, Ghana na Nigeria. Ukiwauliza wanasema taarifa waluzipata kupitia Balozi hapa Doha. Baadhi ya kampuni toka kwao zikaomba tenda zikapata ndo wakaleta watu wao. Sisi Sasa! ukifika hapo ubalozini ukaongea Kiswahili tu wananuna.
UVCCM wanapewa shukrani badala ya watu kuteuliwa kwa uwezo wao ni mambo ya ajabu sana
 
Nimefika Qatar wamejaa watu kutoka Afrika hususani Kenya, Uganda, Ghana na Nigeria. Ukiwauliza wanasema taarifa waluzipata kupitia Balozi hapa Doha. Baadhi ya kampuni toka kwao zikaomba tenda zikapata ndo wakaleta watu wao. Sisi Sasa!ukifika hapo ubalozin ukaongea Kiswahili tu wananuna.
Tanzania Mabalozi waanze kuteuliwa toka sekta binafsi kujaza civil servants na wanasiasa ndio matokeo hayo

Mabalozi wetu wamejaa wanasiasa na wafanyakazi wa Serikali
 
Kuna siku niliwahi kuhoji vigezo vya uteuzi kwa hawa mabalozi sikupewa jibu lolote lenye mantiki zaidi ya kuwa kigezo kikuu ni kuwa kada wa CCM na uwe tayari kupokea maagizo yoyote toka serikalini.
Tunateua mabalozi wazee ndio sababu ya yote haya. Balozini wawekwe vijana tu, sasa unamteua brig mstaafu wa jeshi atafanya nini kule? wao kazi yao ni kuwa military atachee sio balozi, unakuta mzee kashajizeekea so anapachukulia hapo ni sehemu ya kupumzika badala ya kufanya kazi
 
tunateua mabalozi wazee ndio sababu ya yote haya.balozini wawekwe vijana tu,sasa unamteua brig mstaafu wa jeshi atafanya nini kule ? wao kazi yao ni kuwa military atachee sio balozi,unakuta mzee kashajizeekea so anapachukulia hapo ni sehemu ya kupumzika badala ya kufanya kazi
Job description ya Balozi inafananaje?
 
Job description ya Balozi inafananaje?
Sijawahi kuiona mkuu,lakini ni wazi kwamba haiendani na mazingira ya sasa,kuna siku nimemsikia balozi fulani anamlalamikia Magufuli kwamba anakwamishwa na wizara yani balozi anapiga kazi lakini wizara haifanyi kazi kabisa.

Kwa hali ilivo ukute hata hiyo job description haipo,ingekuwepo mleta mada asingeleta hili dukuduku lake zito ambalo limetokana na uzembe wa balozi zetu
 
Kuna siku niliwahi kuhoji vigezo vya uteuzi kwa hawa mabalozi sikupewa jibu lolote lenye mantiki zaidi ya kuwa kigezo kikuu ni kuwa kada wa CCM na uwe tayari kupokea maagizo yoyote toka serikalini.
Slaa alikuwa kada wa Chadema
 
Balozi zetu zimelala sana kwenye fursa za uchumi. Wanachokijua ni diplomasia tu ambayo haileti tija kwa nchi na ulimwengu wa sasa.

Hivi umewahi kujua ajira za walimu wa Kiswahili hapa nchini huko nje zinatolewaje? Nchi zinahitaji walimu kutoka Tanzania lakini wanaofundisha ni kutoka nchi jirani.

Kuna uzembe wa hali ya juu sana kwenye hizi balozi zetu inawezekana watu wanaopelekwa huko hawana uelewa na mambo ya uchumi wa sasa au roho mbaya tu .

Kongole sana kwa balozi wa China anajitahidi sana kutanganza fursa zilizoko huko na kutengeneza nafasi za biashara kwa watanzania.

Mabalozi wetu waache kuvimba na kujiona kama ni Maraisi kwa kuwa wanaiwakilisha nchi, wawatumikie watz na kuwatafutia fursa.

Wawe na utashi na kuthubutu siyo kukalia diplomasia tu eti wanaogopa kuharibu mahusiano ya nchi.Penye kutetea uovu watetee, kama kukaripia wakaripie, mtz ameonewa asemewe na kusaidiwa hizo ndizo kazi zao bana.

Wizara ya Mambo ya nje pelekeni watu wenye uwezo na maono na wanaoijua nchi na vipaumbele vyake. Usishange kwenye balozi kuna wafanyakazi hawajui mlima Kilimanjaro uko mkoa gani, wakiulizwa wanajibu uko Moshi.

Kama balozi zingekuwa zinafanya kazi zake vizuri kwanini vivutio vingi vya utalii na maarufu vilivyopo hapa nchini vijulikane viko nchi jirani???
 
Back
Top Bottom