Balozi zetu toeni fursa kwa Wajasiriamali

Balozi zetu toeni fursa kwa Wajasiriamali

Ndugu zangu huu uzi ni muhimu sana sana. Tuchangie mno na kwa nguvu sana. Inabidi tusikike. Mabalozi wengi wamepewa hizo nafasi ili kumkimbiza uhamishoni aliyetofautiana kimawazo na utawala kwa namna moja au nyingine eti ni ili kuepusha shari. Hii haileti tija hata kidogo kwa Taifa letu!
 
Watanzania ni Roho mbaya tu ndio maana unaona yote hayo yakitokea msitegemee kupata taarifa nzuri kutoka kwa mabalozi na ofisi zingine wamejazana ndugu na mtoto wa fulani hakuna jipya kwa hao watu kutokana na mfumo wao wa upatikanaji...
 
Kazi za balozi ilifaa ziwe zinatoa taarifa nchini za fursa nje ya nchi. Ndo wafanyacho balozi za nchi ya China, kuziuza fursa tele zilizojaa Afrika. Mzungu kastuka Mchina kajaa KILA kona afrika kwa ujinga wa media za western wao wakati wanatangaza habari za negative kuhusu afrika mfano vita, njaa, magonjwa, ukame, umasikini nk media za china zilikuwa zikionyesha positive kuhusu afrika kwamba kuna fursa ya shida ya usafiri wakaleta pikipiki bodaboda zimejaa KILA kona afrika mzima, wakaleta malori na mabus ya kichina KILA kona afrika, wakaleta bidhaa tele toka China, wakaonyeshwa fursa tele za utajiri nje nje mfano madini, nk leo Afrika ndio imekuza uchumi wa china
 
Inashangaza Sana Balozi zetu huko ughaibuni hazitoi taarifa za fursa zilizopo huko. Fikiria nchi za Middle and Far East zilivyo na fursa ya Ajira, chakula na Ujenzi Ila wenzetu ubalozini wametulia tu. Qatar World Cup 2022 inakuja Ila utakuta hawa ndugu zetu hawana huo muda. Why?



View attachment 2169168

View attachment 2169170
Na Waziri husika anashindwa kufanya vikao na hao mabalozi kuelezea sera ya Diplomasia ya Uchumi?

Kwani wanapelekwa huko Nje kufanya nini hasa kama hawasidiiTaifa?
 
Kuna mshkaji alizaa na mzungu bongo mzungu akakimbia kwao na mtoto akakata mawasiliano jamaa akajilipua kuja ulaya bahati nzuri wakati napita mitaani Amsterdam jamaa akaniita nilipondua ni wa home nikampa pesa ya kula kuoga nikampeleka stendi kuu ya mabasi awe analala kujifanya ni msafiri wakati anasubiri pesa afike mji aliko demu wake.ulaya hakuna kupelekana home mtu usiefahamiana nae!

Nikaongea na ubalozi wetu Sweden waje kumchukua wamsaidie wakasema hawana cha kumsaidia na hawakuja kwa siku 5 jamaa akawa mzigo wangu misosi na pesa ya kujikimu!!

Pale stendi kuu Polisi wakamshtukia kuwa sio msafiri wakamkamata wakamhoji na kumuelewa ndo kwa gharama zao wakamsafirisha hadi aliko demu aliezaa nae baada ya kutaja jina wenzetu wana database kila mtu anajulikana alipo kule mji wa demu mamlaka zikampokea na kumuunganisha na demu ambae eti alifurahi kumuona msela!!

Kuna mwaka passport yangu iliisha muda nikapiga cm ubalozi wakaniambia rudi nyumbani bongo karenew!! majibu yao ni short tu

Balozi zetu za ulaya ni takataka staff hawana faida wao ni kuja kwenye sherehe tu mkiwaita ila ukihitaji msaada hawana na wala hawana muda wala nia ya kutafuta fursa kwa watanzania!!

Samia angewabadili mabalozi wote wa zamani aweke wapya na majukumu mapya ya kutafuta fursa anaeshindwa amtoe
 
Tujifunze kwa Majirani. Wakenya, waganda wamejaa Arabuni wakipiga kazi
Dubai na Doha kwa macho yangu nimeona kuna watu wengi weusi wanapiga kazi Airport! Hawa watu wanakuza uchumi kwa nchi zao kwa kutuma mabilioni ya dollar kila mwaka na kufanya uwekezaji mkubwa wa kiuchumi makwao!

Sisi wajinga tukazanie tu kukuza kiswahili , Kiswahili my foot!

Dunia ya ajira na biashara nje ya bongo inatumia English!!Watanzania tunatakiwa kufundishwa na kujua kuongea English kwa ufasaha tangu tukiwa wadogo ili kunufaika na fursa za dunia ya kidigitali na hii inatakiwa ianzie kubadili mfumo wa elimu tusomeshwe in English from primary. Mbona Bimkubwa Samia hatumii Kiswahili kuongea na wazungu kusaka mikopo yao watu wa serikali ambayo wananunulia ma V8?nani atamuelewa kwa kiswahili?

Nyie mazee majinga na makoloni mliopo taasisi ya ukuzaji mitaala na wizara ya elimu hamjui kuongea English fluently na hamuipendi hiyo lugha tunawaomba tufundishieni watoto wetu English as medium of instruction kuanzia primary school wakatafute pesa nje ya nchi kama wenzao wa Kenya, Ghana, Nigeria na Gambia maana serikali ya bongo ni maskini na inawadidimiza raia kwenye umaskini kwa matozo kibao na vibanda vyao mnavunja, mmeshindwa kuzuia mfumko wa bei , mmeshindwa kutengeneza mazingira ya ukuaji wa sekta binafsi inayoajiri watu nk

Nyerere alikazania tufundishwe kwa Kiswahili ili tusiweze kufanya kazi nje atutawale vizuri. Nyerere alipenda watanzania wawe maskini awatawale mpaka afe abaki kutukuzwa! Nyerere kafanya mengi mazuri mno ila kwa hili siko nae.

Wenye akili tu watanielewa!
 
Back
Top Bottom