Hao hawatakiwi hekima wala kubembelezwa. Wana msemo wao mmoja kuwa hawataki kupoteza mteja.
Wakati nafanya kazi serikalini nilipata msiba wa mzee. Msiba ule ulikuwa wa ghafla sana nikatakiwa nisafiri toka kanda ya ziwa to nyumbani Mtwara nami ndio mkubwa ikabidi niongeze nguvu kidogo.
Nikaenda wanikope 1,200,000 na wakaingizia makato kwenye mshahara wangu na nilikubaljana nao niilipe hiyo kwa miezi 6. Kweli wakaingiza mzigo nikiwa nyumbani na ulinisaidia kwenye msiba hadi ukaisha fresh.
Baada ya mwezi 1 nikapata pesa yao nikasema niwarudidhie na wanitoe kama mteja wako. Ilikuwa ni mbinde, nikasema hawa nikiwachekea hawatanitoa. Niliwawashia moto pale Mwanza mpaka wakanitoa na HRO nae akawawashia moto kuwa hataingiza makato ya mtu mwingine toka kwenye taasisi yetu awe mteja wao hadi wanitoe.
Usiwaendekeze, kawawashie moto watakutoa wapuuzi hao.