Banc ABC wamekataa kulipwa, msaada wenu unahitajika

Nenda pale BOT mkuu.

Hizi bank si rafiki kwa wakopaji. Ukichelewesha jau
Ukiwahisha jau
Hawana jema
 
uza deni hilo aidha kwa CRDB,NMB au bank yeyote alafu utawalipa hao walionunua hilo deni.

Hivyo Bank ABC watalipwa na bank husika sio wewe tena.
 
Banc ABC na Bayport, tofauti yao ni majina tu. Ukikubali kuingia nao mkataba, basi utambue fika maelekezo waliyokuambia kupitia mdomo, ni tofauti kabisa na yale ya kwenye mkataba wao.

Pole sana mtoa mada.
 
Nakuhakikishia mrejesho nitaleta maana wamenisumbua mno.
 
Bank inakutumiaje nyaraka Whatsapp.

Mtaalam kusanya document zako hakikisha Watu zaidi wanajua hili ndani ya bank na upande wako.

Pia tumia email mara zote kwenye mambo ya kiofisi
Ndiyo maana nilikuwa na mpango wa kuanzia mahakamani kufungua shauri la madai ya mkataba hard copy.
 
Hapa Tanzania ukitaka upewe huduma kwa haraka bila kubabaisha jitahidi sana siku ya kwanza kabisa waseme "HUYU MTEJA/JAMAA SIO MWELEWA"... Ukiwa mstaarabu utaonewa sana. Kwenye biashara hakuna kuoneana huruma wala haya. Wakikuona sio mwelewa siku nyingine ukienda watakuhudumia haraka ili kuepusha shari.

Halafu wewe ni mfanyabiashara wa aina gani unachukua mkopo wa miaka miwili na kurejesha ndani ya miezi mitatu? Ina maana biashara yako haikuhitaji kukuzwa zaidi? Au uli-bet ukapata hela ya kulipa? Wewe pia upande wako kuna ukakasi. Benki kukataa kulipwa hela zao zote na riba ya miaka miwili ndani ya miezi mitatu watakuwa hawana akili timamu. Hiyo hela yako ukiwapa mapema wataizungusha tena na kupiga hela zaidi. Mteja anayelipa fasta huwa anapendwa mno na mabenki.
 
Nilichukua pesa yao nikaweka kwenye biashara yangu ya uchuuzi wa mazao, yaani miezi miwili tu kwa kuzungusha kijijini kuleta mjini tayari nimepata faida na mtaji umesimama,

Si unajua huku tunaishi na mazao ya msimu
 
Nenda BOT mkuu kila mkoa wapo alafu usiwe mstarabu sana sometimes jifanye fyatu fyatu nchi ngumu hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…