Mnasubiri nini kumkaribisha Advocate Mwabukusi,kwenye majukwaa yenu?
Katika kupigana vita huwa hatuchaguwi ni nani rafiki,bali Urafiki unakuja "Automatically"sababu wote mnaojikuta upande mmoja wa vita mkipigana bega kwa bega dhidi ya Upande wa pili wa adui yenu.Tayari...
Nyinyi mnakuwa ni zaidi ya Marafiki bali kama ndugu kabisa.
Hii ni kwa sababu mnakuwa mmeingia hiari kufa pamoja katika uwanja wa Vita.
Mkiwa mnatetea kile mnachokiamini katika umoja wenu, dhidi ya yule mpinzani wenu.
Pia Rafiki anahitajika kwa kuzingatia kwamba urafiki ni moja ya mali ya thamani sana katika maisha yetu.
Hili la DP-WORLD limegeuka kuwa uwanja wa harakati za mapambano dhidi ya wadhalimu kadhaa, wanaotaka kuuza au kugawa raslimali za nchi yetu kwa faida zao binafsi ambazo bila shaka wanazijua wao.
Dhidi ya wazalendo wa kitanganyika wanaokataa kushuhudia nchi na maliasili zake, ikitumika vibaya na kundi dogo la wenye mamlaka serikalini kwa maslahi yao binafsi pamoja na maswahiba wao.
Ni katika suala hili ambapo wameibuka watu wazalendo kama Advocate Mwabukusi akiwa sambamba na kada maarufu wa "CHADEMA" maarufu kama Mdude Nyagali.
Sina haja ya kuwaelezea wawili hawa kwa sababu tayari wameingia katika orodha ya watu wenye uthubutu wa kupambana na dola kwa hoja zenye mashiko.
Ushauri wangu kwa "CHADEMA" ni kwamba huu ungekuwa wakati sahihi wa kumkaribisha rasmi Mzalendo Mwabukusi.
Ili awaongezee nguvu katika vuguvugu linaloendelea la mapambano ya kuokoa Bandari zetu na kuidai katiba mpya ya JMT.
Fanyeni usajili mpya bila kuangalia maslahi yenu binafsi bali uzalendo kwa maslahi mapana ya Tanganyika yetu.
Na hii itachagiza pia CHADEMA kuendelea kujisimika vizuri kwenye maeneo ya Nyanda za juu kusini huko.
Mwabukusi tayari ni Potential huko kusini....
za kuambiwa ongezeni na za kwenu.
Siasa ni pamoja na mikakati mizuri katika kuunda team sahihi katika wakati sahihi.
Cc:
Erythrocyte