Bandari mambo mazuri kuliko tunavyofikiria. DP World

Bandari mambo mazuri kuliko tunavyofikiria. DP World

FaizaFoxy

Platinum Member
Joined
Apr 13, 2011
Posts
100,246
Reaction score
123,145
Hili sakata la Bandari zetu limenifanya niingie kwenye utafiti kidogo, niliyokutana nayo mwenyewe nikacheka peke yangu. Jifunzeni kutafuta fursa.

Tukitaka tusitake ni lazima bandari zetu ziendeshwe na mashirika makubwa ya kuendesha bandari duniani kwa masharti yao.

Hatuna ujanja, sisi tujihakikishie tu tunafanya haraka kuzitumia fursa kadri tunavyoweza.

Bandari zetu kuendeshwa na nani au nani imehaamuliwa zamani.

TICTS hawakuondoka kwa ujanja wetu au uhodari wetu, misheni yao imekwisha.

DP World haipo kwa ujanja wetu wala ujinga wetu, wapo kwa makusudi kabisa na wanaelewa nini cha kufanya.

TICTS ndiyo haohao Hutchison, Hutchison ndiyo haohao AD Ports, AD Ports ndiyo haohao DP World.
. Wameshagawana zone za kazi. Ni mengi sana, mapoyoyo hamuwezi kunielewa.

Bei za kutulipa zimeshaamuliwa na zipo tayari siku nyingi, wana vigezo vyao havibadiliki, vinapishana kidogo tu kutokana na operating costs zao.
.
Sisi tutafaidi na wao watafaidi.

Mtajionea kimya kimya kuanzia mwaka huu machafuko ya Congo yamekwisha, machafuko ya Sudan Kusini yanakwisha. Gas Tanzania inaanza kuchimbwa kwa kasi, uchumi Tanzania unabadilika ukuwaji kasi ya ujywaji itaongezeka sana mwakani.

Mashamba makubwa yataibuka, mabarara, umeme, usalama, mahosoitali yataongezeka na kuboreshwa.

Tunachokitaka tutakipata kiwepesi sana. Wajinga wajinga kama Magufuli hawatokubalika tena kwa miaka mingi ijayo.

Tujitayarishe kupokea Wakubwa wa nchi za UAE, Oman, Saudi Arabia, Qatar. Kwa uchache.

Kila mahali patakaa sawa.

Uliza chochote utakacho, yote ninayiyaandika yana ushahidi.
 
Hili sakata la Bandari zetu limenifanya niingie kwenye utafiti kidogo, niliyokutana nayo mwenyewe nikacheka peke yangu.
jifunzeni kutafuta fursa.
Nimekuelewa, na ningekuelewa bila.hata kutupa insults. Ni kweli kufanikiwa kuna njia mbili ukaribishwe kwenye meza ya wakuu au upigane kupata nafasi kwenye meza ya wakuu.

Route yetu imeshakuwa hii ,tinavumilia mpaka tunaingia kwenye meza za wakuu. Hayati JPM aliamini angeweza kupigania nafasi hiyo katika meza ya wakuu..nayo ni njia sahihi pia.

Kilicho chema hata hao wakuu wamejifunza kuwa Sio wote watanzania watangojea wako wenye akili ya kupigania nafasi, trust me hawatutazami kama zamani..na huenda haraka ya kutusogeza kwenye meza kuu imechangiwa na Hilo.

Asante sana kwa mtazamo chanya FaizaFoxy
 
Hili sakata la Bandari zetu limenifanya niingie kwenye utafiti kidogo, niliyokutana nayo mwenyewe nikacheka peke yangu.
jifunzeni kutafuta fursa.

Tukitaka tusitake ni lazima bandari zetu ziendeshwe na mashirika makubwa ya kuendesha bandari duniani kwa masharti yi.
Nakuomba inbox
 
CONGO inabidI ifunguke, bandari moja haitoshi, Congo ni kubwa sana. Mali za kuingia na kutoka Congo ni nyingi sana. Bandari ya Dar itakuwa busy 24/7 bandari ya Mombasa pia itakuwa busy sana. Itabidi ya Bagamoyo ijengwe haraka. Haya ni kwa huku mashariki, kwa magharibi Tsysri AD Ports wanajenga bandari kubwa Congo. Hao. Ni Abu Dhabi Ports, siai hapa ni Dubai Ports. Mombasa itakuja tu kampuni. Nyingine. Lkimi. Ndiyo hawahawa wamoja. Bagamoyo anapewa mwengine lakini ndiyo hawahawa.

Dollar million 500 ni kwa ajili ya TEHAMA tu.

Biashara itayofanyika hapa hata kuwekeza wao tutakuwa hakuna umuhimu, bamdari itaingiza pesa nyingi sana.
 
Kile kitendo cha Rais kusema Mifumo haisomani kati ya TPA na TRA tu hapo nikajua kuna Mchwa weusi wanajilia pesa miaka mingi huku bado Quality of services bandarini ni poor.

Sasa ni muda muafaka kuwakaribisha DP world kutusaidia sisi wafanya biashara ku import mizigo yetu kwa haraka wakati huo Kutakua na fursa za ajira na gawio la faida serikalini lililo wazi.
 
-Vipi ishu ya bandari kupanda thamani?
-Vipi ishu ya mbia wetu kushindwa kulekeleza yalipo kwenye mkataba na bado akaendelea kuwepo, kwasababu mkataba unambeba?
-Hivi unahisi kwa matrilion yanayoibiwa kwa mwaka Tanzania tunashindwa kuendeleza bandari, mfano DP world wanawekeza dola million 500 ambayo nisawa kwa mwanzo je linganisha na pesa zilizoibiwa mwaka jana 2,zaidi ya trillion 2?
-Kama hatuna wataaalamu je chuo cha bandari na maprofesor wake wanafanya kazi gani?
-Kwanini tusilete wataaalamu na technologia changamfu na basic tukabaki na bandari?
-Kwanini tuuze bandari bila ukomo na kuziwepo room ya kujitoa kwasababu wanadamu hubadilika wakitubadilikia tutamlaumu nani?
-Kwanini wenye nchi wasisikilizwe wananchi kwani bandari ni ishu ya kifamilia?
-Kwani kama sisi ni kizazi cha kijinga tumeshinda kufanya kwa uadilifu,kwanini tusiviifadhi kwa vizazi vijavyo kwa sababu katikati ya wajinga yamkini akawepo mwelevu hata mmoja,kwani nyerere asingeviifadhi wewe ungevikuta?
-Watoto wetu watafaidi nini?watajivunia na nini? Kama tunaangalia leo tu?
-Trillion 26 ya mwaka 2023? Ni dawa kithamani na trillion 26 za mwaka 2070?2100 ? 3000?
- unaonaje tukatoa rangi ya njano,kijani,na blue kwenye bendera ya taifa ukabaki nyeusi kwasababu migodi tumeuza,misitu tumeuza na ardhi ,na Bahari na maziwa ndo tunauza hivyo yani,
Mwisho wewe unalipwa shi ngapi? Kuteteza huu ufuska?
 
Faiza hana uzalendo wowote wa kuitakia Tanzania mema. Faiza ana ajenda pekee na Uislamu kuliko chochote.

Ukiona Faiza amelivalia dera swala lolote, tambua ya kuwa kuna ajenda ya siri juu ya Uislamu umefichwamo.

Bahati mbaya sana, ameacha kuwa Mwalimu wa 'huko shule mlienda kusomea ujinga' na kugeuka kuwa Mwanafunzi mjinga asiye na uwezo hata kidogo. Anaandika pumba, anakosea maandishi.
 
Back
Top Bottom