-Vipi ishu ya bandari kupanda thamani?
-Vipi ishu ya mbia wetu kushindwa kulekeleza yalipo kwenye mkataba na bado akaendelea kuwepo, kwasababu mkataba unambeba?
-Hivi unahisi kwa matrilion yanayoibiwa kwa mwaka Tanzania tunashindwa kuendeleza bandari, mfano DP world wanawekeza dola million 500 ambayo nisawa kwa mwanzo je linganisha na pesa zilizoibiwa mwaka jana 2,zaidi ya trillion 2?
-Kama hatuna wataaalamu je chuo cha bandari na maprofesor wake wanafanya kazi gani?
-Kwanini tusilete wataaalamu na technologia changamfu na basic tukabaki na bandari?
-Kwanini tuuze bandari bila ukomo na kuziwepo room ya kujitoa kwasababu wanadamu hubadilika wakitubadilikia tutamlaumu nani?
-Kwanini wenye nchi wasisikilizwe wananchi kwani bandari ni ishu ya kifamilia?
-Kwani kama sisi ni kizazi cha kijinga tumeshinda kufanya kwa uadilifu,kwanini tusiviifadhi kwa vizazi vijavyo kwa sababu katikati ya wajinga yamkini akawepo mwelevu hata mmoja,kwani nyerere asingeviifadhi wewe ungevikuta?
-Watoto wetu watafaidi nini?watajivunia na nini? Kama tunaangalia leo tu?
-Trillion 26 ya mwaka 2023? Ni dawa kithamani na trillion 26 za mwaka 2070?2100 ? 3000?
- unaonaje tukatoa rangi ya njano,kijani,na blue kwenye bendera ya taifa ukabaki nyeusi kwasababu migodi tumeuza,misitu tumeuza na ardhi ,na Bahari na maziwa ndo tunauza hivyo yani,
Mwisho wewe unalipwa shi ngapi? Kuteteza huu ufuska?