Bandari ya Bagamoyo aka Mbeganizhou ya Wachina

I think you are an idiot
 
Propaganda za Kupinga Maendeleo ni kubwa sana.

Wachina ni washirika wetu wakubwa, tumeshirikiana nao katika kila sekta kuanzia Jeshini, Elimu, Afya na Kisiasa.

Mradi ungekuwa Chato au kanda ya Ziwa ungefanywa haraka sana. Kuzuia 2016 mara 2018 unaruuhusu ujengwe baadae 2019 kigeugeu tena unazuia. Hiyo ni kuonyesha maslahi ya Sukuma Gang yalibinywa.

Miaka 33 au 66 ama 99 ndio Sheria ya Ardhi ya Tanzania Lease ndio muda wake, Propaganda kuwafanya Watanzania ambao tumewanyima kumiliki ardhi waone kama vile wameibiwa.

Watanzania wanataka Ajira, wanataka biashara wanataka kusonga kwa speed sio kutuletea sera za Magufuli za wakati wa Vita Baridi

Never and Never again
 
Ndo kilichofanyika kuwaambia watoe hivyo vipengele nyonyaji. Hawajarudi tena ujue kuwa nchi ilikuwa inauzwa
 
Yawezekana wa China walikwishahonga fedha nyingi sana na zikatumika hata kwa 2015 campaign bila mhusika mkuu kufahamu.

Yawezekana Pia wachina na wa-Oman walianza kudai fedha ya kifunga uchumba walotoa kwa mwezeshaji au facilitator baada ya kuona mkataba umevunjwa na fedha zimeliwa.

Au Pia yawezekana mwezeshaji alianza kuona hali inakuwa mbaya maana muda unazidi kuyoyoma na kelele za "aendelee" zilianza kushika kasi.

CCM ikibanwa na wananchi kwenye hii haichomoi 2025.
 

Afu hivi mbona pia hatajwi mu Oman ‘Mwarabu’ ambae nae nasikia anatoa pesa hapo kwenye huo mradi au mchango wake ni mdogo sana ?
 
Bunge la CCM lihojiwe na wananchi kuhusu mkataba wa bandari ya Bagamoyo.

Je, wachina na mu-Oman walitoa fedha za awali au la na kama walitoa fedha hizo walitoa kwa nani na zimetumikaje.

Jana nilitarajia msimamo tofauti wa upinzani kupitia Freeman Mbowe lakini aliniacha "very disappointed".
 
Afu hivi mbona pia hatajwi mu Oman ‘Mwarabu’ ambae nae nasikia anatoa pesa hapo kwenye huo mradi au mchango wake ni mdogo sana ?
Haya masuali ndo msingi wa kutafuta ukweli.

Vinginevyo ni propaganda zisizo na tija.
 

Kwa akili yako unaamini Rais angetaka kitu angekosa?! Kweli akili yako fupi[emoji38]
 
Haya masuali ndo msingi wa kutafuta ukweli.

Vinginevyo ni propaganda zisizo na tija.

Maana tunasikia ni Mchina tu mara atachukua ardhi/ bandari wakati nasikia pia kuna hao wa Oman pia wanaweka pesa yao sasa mbona kelele kwa m China tu

Kama ulivyo shauri utafutwe ukweli na hiyo mikataba iwekwe wazi mwisho wa siku kama Taifa tutaona tuingie au la
 
Kiukweli Magufuli tutamkubuka,hizi mbuzi zinataka kututoa kafara,ipo vipi tutageuka Somalia kama huu upumbuvu wa hivi utafanyika. Sometimes bora kuendeshwa na Jeshi tu.
 
Yawezekana mkataba ulisainiwa na fedha za awali zilitolewa

Wa kuulizwa hapo ni AG na waziri wa Sheria wa awamu ya 4
 
We Ngaliwe naona umeanzisha mradi wako wa upotoshaji kwenye jukwaa hili.

Kila wakati unaanzisha thread za kupotosha tu!

Bahati nzuri,uongo huwa haudumu. Ukweli kuhusu mradi wa Bandari ya Bagamoyo utajulikana tu. Na wewe na wapotoshaji wenzio mtapata aibu kubwa!
 
Unalipwa hela ngapi kuleta haya mauongo yako hapa?

Umejaza hoja za uongo kila mahali!

Ndio maana hilo andiko lako lilikuwa limetupwa,halina thamani yoyote! Ni takataka kabisa!
 
Wewe ndiye mjinga!

Watu wanaojitambua hawawezi kupinga mradi wenye manufaa makubwa ya kiuchumi kwa nchi kama Bandari ya Bagamoyo kwa sababu ya chuki binafsi na faida za kisiasa.

Mradi ule unahusisha bandari kubwa ya kisasa yenye kufungamana na industrial parks kibao na hivyo kuifanya Tanzania kuwa lango juu la nchi zaidi ya nane za Afrika.

Mradi huo ungejengwa na wachina/waarabu wa Oman kwa gharama ya dola bilioni 10 kwa utaratibu wa concession hivyo serikali haitumii hata thumuni ya mlipa kodi. Siyo mkopo. Wanaendesha bandari kwa kipindi tutakachokubaliana huku wakichukua port charges kisha wanakabidhi kwa serikali.

Mbona hata Bandari ya Dar inaendeshwa kwa utaratibu huo na TICTS ya akina Karamagi?

Hebu acheni figisu zenu nyinyi wazalendo uchwala mnaosumbuliwa na ajenda zenu za siri! Badala ya kujadili hoja mmekalia kujadili na kuchafua watu.
 
Umenena vyema!

Unawatukana wachina wakati hata pesa za kujenga Tazara na Urafiki hatujawalipa! Hawa watu wanaowaza kizamanizamani sijui wametoka wapi nchi hii?

Hawa wachina mnaowatukana ndio wabia wakubwa hata kwenye mradi wa bomba la mafuta uliosainiwa jana kule Uganda!
 
Mwenye hilo Bunge kafa kamuachia Ndugai sasa hao Wachina wanahangaika nini Wamuhonge Ndugai kitita kinono ili mgogo akafe kwa kula starehe

Ubinafsi wa KiCCM ndio umetufikisha hapa

Hata Mama akikomaa atashinikizwa
Huna pa kushika sasa umekata tamaa
 
Wachina hawapo tayari kwa hilo,wanataka watekeleze kama ulivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…