Swala la mradi wa bagamoyo mtu alieona mkataba huo ni Rais Magufuli tu, na huyu mtu alikua na sifa tatu kuu "MUONGO, MSIRI NA FISADI".
Hii DNA ameiacha mpaka kwa baadhi ya wateule wake waliobakia madarakani. Mmoja wao ni Waziri Mkuu (Ambaye tunatakiwa kumwanzishia amsha amsha mitandaoni AJIUZULU).
Swala la mradi wa bandari ya bagamoyo hao wote mliowataja hapo (Kina Zitto, Prof Assad na wengine - wamesema wazi hawajaona FEASABILITY STUDY YA HUO MRADI, na wanaomba iwekwe wazi kwa wananchi wajionee kama ni kweli Mkataba ni wa miaka 99).
Serikali ya Rais Magufuli ilikua hasikilizi ushauri, iliendekeza uongo/ufisadi/propaganda/uonevu na ndio maana haikuwa wazi kiutendaji:
Mfano,
Kutokana na Mkaguzi & Mdhibiti Wa Hesabu Za Serikali (CAG Kicheere) Ndege zilizopo zimeingiza hasara ya Sh. Billioni 60, wanaona hio hasara haitoshi wameamua kuongeza ndege pengine hasara ifikie hata Sh Billioni 100.
CAG Mstaafu Prof Assad alisema "Shirika la ATCL linadaiwa madeni mengi sana na alifanya kuishauri serikali shirika hilo la ndege ATCL lifilisiwe kwanza kimahakama ili madeni yalipwe hela kidogo itakayo patikana ili hayo madeni yafe (Kwa kuuza majengo wawili ilionayo), au lasivyo wanaodai watakamata ndege zikinunuliwa, likifilisiwa kimahakama halafu wafungue shirika la ndege jipya ndio wanunue ndege nyingine mypa, na wasinunue kwa hela cash".
Kuchamba kwingi na kujifanya wajuaji, wameamua kununua ndege nyingine 3 wakati wameambiwa kwamba shirika linaendeshwa kwa hasara, hii haihitaji hata elimu ya darasa la saba kufahamu, halafu kuna mpuuzi anasimama bungeni anasema eti kuboresha usafiri wa anga.
SWALI KWA WAZIRI MKUU:
1) Huko ni kuboresha usafiri wa anga au kuboresha hasara ya taifa likuwe zaidi???
2) Ndio tuseme bado anatuona watanzania "MAJUHA/WAPUMBAVU/WAJINGA" kuendelea kutudanganya kwamba wanaboresha usafiri wa anga wakati shirika ni marehemu mtarajiwa???
3) Kununua hizo ndege 3 mpya ni kujitoa ufahamu ili "KUMKWAMISHA NA KUMHUJUMU" Rais Samia ili aonekane yeye ndio hakujali mahesabu ya CAG na kuendelea kuingia kichwa kichwa kumunua ndege au vipi???
#WaziriMkuu-AJIUZULU.
#MamaSamia VUNJA BARAZA LA MAWAZIRI LOTE (Wanakuhujumu).