Bandari ya Bagamoyo aka Mbeganizhou ya Wachina

Bandari ya Bagamoyo aka Mbeganizhou ya Wachina

nchi yenye miaka zaidi ya 50 ya Uhuru.
Yenye watu million 60 +.
Bado wanategemea bandari moja ya dar?..
MTU akiwa na bidhaa zake akitaka kupeleka Zanzibar mpaka apande JAHAZI?..
Ukitaka kwenda Zanzibar ukiwa bagamoyo NI mpaka uende bandari ya dar.
Bandari ya bagamoyo itarahisisha biashara nyingi Sana.
Kwahiyo unateseka bandari kuwa Dar...!?tafakari kwa kina...
 
Fanya safari uende pale bagamoyo kwenye kile kibandari mshenzi.
Uone bidhaa zinazopelekwa Zanzibar.
Cha ajabu mpaka leo wanatumia JAHAZI la SHUKA na injini .
Ni Jambo la AIBU
Kwahiyo unateseka bandari kuwa Dar...!?tafakari kwa kina...
 
Montenegro wana deni la 1$bl ambalo waliingia na wa China na wameshindwa kulilipa. Wanalazimika kulipa ardhi yao yenye thamani hiyo[emoji848]!
Huu ni mkopo bagamoyo port sio mkopo ni uwekezaji na ulisanifiwa 2004 wakati wa utawala wa hayati Mkapa
 
Makubaliano yao unayajua?
Ndio maana tunataka mkataba wa bandari ya bagamoyo iwekwe wazi ili Wananchi wajiridhiishe kwanza.
Vinginevyo ni porojo tu.
Hakuna serikali yoyote duniani ambayo inaweka mkataba wazi inayoingia na nchi nyingine. Mtasubiri sana.
 
Ujenzi wa bandari ya bagamoyo umejaa uhuni wa kutisha.

Kulingana na mkataba, wachina walitaka kuingia makubaliano ya kujenga miundombinu yote ya bandari kwa gharama zao.

Serikali ya Tanzania haikutakiwa kuchangia senti yoyote kwenye ujenzi.

Wachina walitaka kujenga bandari yote kwa gharama zao.

Baada ya bandari kukamilika ujenzi wa miundombinu yake, mkataba unasema kwamba, Wachina wanapaswa kuchukua mapato yote ya bandari kwa MIAKA HAMSINI.

Kwahiyo, baada ya miaka hamsini ndio watakapowaachia bandari yenu.

Baada ya Wachina kukomba na kufaidi mapato yote, ninyi mtakabidhiwa bandari yenu mwaka 2070.
 
Ujenzi wa bandari ya bagamoyo umejaa uhuni wa kutisha.

Kulingana na mkataba, wachina walitaka kuingia makubaliano ya kujenga miundombinu yote ya bandari kwa gharama zao...
Then kwa miaka 70 hiyo watakuwa wanalipa kodi? Na kama ni hivyo kodi kiasi gani?

Unaweza ukaja kwangu una mradi wako, nikakupa aedhi uweke mradi wako. Terms zangu ni kuwa you will have to abide by tax regulations of my specification.

Ingiza gharama zako, mimi bila kujali unapata nini, utanilipa kodi kwa chochote utakachokifanya s per tax administration laws za kwangu.
 
Eti hatuna uwezo wa kuijenga bandari hiyo hivyo tuwaite waje kutujengea kwa masharti yao, mfyuuuuuu [emoji35]! Yaani yaliyoitokea Zambia hayajawashtua, haya ona ya Montenegro nako!
Kama nchi yetu haina uwezo wa kuijenga bandari yenyewe basi kwa sasa hatuihitaji hiyo bandari! Tutakapoihitaji tutaijenga wenyewe bila kutegemea mjomba fake[emoji35]!
binti acha kufyonya ovyo.
 
Rais Magufuli aliukataa uhuni kwa niaba ya watanzania. Ametangulia mbele ya haki ni jukumu letu watanzania kuchukua lindo la rasilimali zetu.
 
Rais Magufuli aliukataa uhuni kwa niaba ya watanzania. Ametangulia mbele ya haki ni jukumu letu watanzania kuchukua lindo la rasilimali zetu.
Magufuli alishasema mkataba huo ni labda mtu asiyejielewa ndiyo anaweza kuuingia
Sasa hawa wanaoupigia chepuo si wauweke
Wazi nao raia wauone, wasituingize chaka

Ova
 
Ujenzi wa bandari ya bagamoyo umejaa uhuni wa kutisha.

Kulingana na mkataba, wachina walitaka kuingia makubaliano ya kujenga miundombinu yote ya bandari kwa gharama zao...
Mataga kazi mnayo ila mnasahau kuwa tayari mama Samia ndiye rais wa JMT na hakuna mjadala.
 
Back
Top Bottom