Mmawia
JF-Expert Member
- Aug 20, 2013
- 122,494
- 96,074
Nakubaliana na mawazo yako mazuri kama wewe.Hili ndio tatizo lilipo, mahaba ya vyama na itikadi za kisiasa, chuki au mahaba juu ya mtu fulani.
Huu mradi nahisi kuna watu wanaweza kuukubali au kuukataa kwa sababu tu JPM aliupinga. JPM is no more na hatarudi tena kuishi kwenye hili taifa so kama kuna hasara au faida itapatikana na ya sisi tuliopo sasa na watakaokuja baadae so maamuzi yetu yawe juu ya facts sio hisia na mihemko ya sijui Mataga na Machaga...
Ila ukweli unaoligubika hili suala ni la kundi fulani kusema kwa sababu mwendazake aliukataa huu mradi basi usijengwe.
Hapa hili kundi linatufanyia sivyo maana mwendazake alikuwa na mtazamo wake kama binadamu.
Binadamu atabakia kuwa binadamu na lazima awe na mapungufu yake pia.
Kama taifa lazima tufungue macho mbele zaidi juu ya huu mradi badala ya kutegemea na kuamini mawazo ya mtu mmoja.