Bandari ya Bagamoyo Ijengwe au Isijengwe? Soma Makala hii Tujadili

Umepata milo yote mitatu ama unabwabwaja tu hapa na bundle lako la week?
 
Naona watu wengi hilo neno Bagamoyo ndio linawakera sana. Hebu tuondoe neno Bagamoyo libakie ujenzi wa Bandari mbadala mtazamo wako utabakia huo huo kama wa JPM?

Je unadhani kwa mahitaji yetu na nchi zinazotuzunguka bandari ya Dar inatosha? Ukishajibu hilo swali ndio tunaweza kujadili au kuacha kujadili kabisa.
 
Ndio mlivyoaminishwa na mwendazake! Ndio maana kila ofisi akawajaza wana usalama wengine hata hawajui kufanya hizo kazi mahala wanapowekwa hadi wanastukiwa mapema na hawapati walichopelekewa kufanya
 
Ijengwe, lakini kwa ubia kati ya serikali na mwekezaji na kila kitu kuanzia mkataba, fidia, mapato, kodi, nk viwe WAZI KABISA bila kificho.
Haya hapa masharti kwamishi ya ujenzi
(Tafadhali jadili masharti badala ya kumwangalia Kakoko)
 
Bandari ya Bagamoyo isijengwe ziendelezwe za Tanga, Dar na Mtwara. Zote hizo tatu zinafanya kazi za kimkakati kiuchumi.

Ile ya Mtwara inalo soko kubwa la Malawi na Zambia. Hii ya Tanga inalo sokoni kubwa la kaskazini na hii ya Dar ndio kongwe na muhimu kuliko hizo mbili zilizobaki.

Hayo matakwa ya uwepo wa bandari ya Bagamoyo kwa namna yanavyoelezwa kwa mapana itakuwa na madhara makubwa miaka mingi ijayo kwa usalama mzima wa Tanzania.

Mheshimiwa wa Kongwa kama katumwa na wachina, aende akawambie wanachokitaka hakiwezi kuja kufanikishwa.
 
Ndio mlivyoaminishwa na mwendazake! Ndio maana kila ofisi akawajaza wana usalama wengine hata hawajui kufanya hizo kazi mahala wanapowekwa hadi wanastukiwa mapema na hawapati walichopelekewa kufanya
Wewe ndiye unajiaminisha kile ulichoandika hapo unajiona umetumia akili kumbe ni kutoa hewa chafu ya nafsi.
 
Bandari ya Dar haina eneo la kutosheleza mahitaji ya huo mradi
Watakuja kujenga vitukuu vyetu, tusiuze nchi kwa wachina! Waafrika sijui tukoje? Unsmps MTU miaka 99!! Atajenga miundombinu anayojua kuwa itadumu kwa miaka 100 tu. Baada ya hapo anakukabidhi mradi ulio-expire tayari na uwezo wa kuukarabati huna.!! Ukishindwa anakuomba umpe miaka mingine 99!!
Ni kama tulivyopigwa pale mlimani city! Pale hakuna jengo la kuhimili miaka 99. Chuo kikuu wanasubiri kikabidhiwa hewa!!
 
Yaani mie nashindwa kuelewa, watz mnapoteza nguvu nyingi kudebate miradi ambayo mikataba yake hamuijui...bali imebaki kuwa kama ' hearsay' tu... oooooh mara mkataba ni mbovu, oooooh mara ni mzuri...si uwekeni mezani wahusika/ wabunge/watu waupitie, na ndipo tujue ' mbivu au mbichi'...hizi longolongo nyingi mwisho wa siku hazitusaidii...
Katiba hairuhusu, mkataba ni siri kali🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣😤
 
Hizi zoote ni ngonjera, leteni mkataba tujue mbivu na mbichi... Nani msema kweli nani muamba ngoma.
 
Kama kuna mtu aliyeelewa hii post anifahamishe. Blah blah nyingi. Rais Magufuli hawezi kuzuia maendeleo hata kidogo. Kuna kasoro kubwa sana ndio maana haikuendelezwa. Tuache ushabiki na mzee wa msoga akae kimya
 
Mkuu Kilatha kumbuka hizo $10B ni part ya FDIs inflow... Kwa Mtazamo wangu tungeangalia terms za huo Mkataba
Hizo $10B utajuaje Kama wamewekwze hicho kiasi ili hali amna uwaz wowote na umeshaambiwa amna kuingiliwa ,wanawezi kutumia hata $5b wakakwaambia wamitumia $ 11B na huwezi bisha

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Ila hayatuhusu, ni vema tungeingeza nguvu kwa wake zetu na mkate wa kila siku kuliko huku ambako Ndugai ilikwisha chukua chake
 
Watanzania hata masharti yote tunayoyataka kwao wakitutekelezea,bado bandari zingine zitakufa kifo cha mende,sababu ni ufanisi wa wenzetu katika bandari.Lazima zife hatuna namna.
Zikifa si ndo kutakuwa na monopoly ya bagamoyo pot na ndio lengo hasa ,ukishaaua hizo bandari maana yake umwaua ajira za vijana wa kitanzania na kodi kem kem ,kwa machina hutaweza kukanyaga kudai hiyo kodi maana mashart ya mkataba ni Kuwa asiingiliwe na amna TRA kutia mguu hapo

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Kama kwenye mkataba kuna kipengele kinacho zuiya bandari zingine zote zisifanye kazi, kipengele hicho tu kinatosha kufanya mkataba kuwa batili maana nikuuwa uchumi.

Kabla sijauona mkataba nadhani kwa %85 lazima kunazuio la bandari nyingine kufanya kazi mara hiyo ya wachina itakapokuwa imekamilika.

Sababu mchina atataka mizigoyote ipitie kwake ili arudishe garamazake na faida.

Kifupi bandari ya mchina isijengwe.
 
JK alianza mazungumzo ya awali na Chinese 2012 kwa ajili ya kujenga Bagamoyo port kama alivyo ujenzi wa SGR, mazungumzo ya awali ilitakiwa wapewa Chinese.

Alipoingia JPM akapata term nzuri kwa ujenzi wa SGR toka Turkey kwa gharama ambazo ni competitive kuliko China. Nadhani wengi tunaelewa China kajenga SGR ya diesel Kenya kwa gharama kubwa kuliko SGR ya umeme ya Tanzania;
Kwa msingi wa kuvunja mkataba wa awali wa SGR na kumpa deal mturuki, kwa simple logic kuna terms huenda hazikiwa sawa au kuna jambo ambalo huenda lilikuwa limefichina na JPM bila shaka aling'amua.

Kenya’s difficulties in servicing its debts for the newly-built, Chinese-financed Standard Gauge Railway (SGR) is nearing a breaking point.

Kenya miaka ya majaribio kuendesha SGR haikulipa, ndio maana phase 2 Mchina alikataa kutoa hela ili SGR ifike mpaka Uganda

Tanzania tukubaliane tumekuwa tukisaini mikata mingi hususan kwenye madani, baadae tunajikuta "tumepigwa". China alikuwa ni kila kitu kwenye ujenzi wakati wa JK, nadhani JPM alikiwa sawa kushindanisha tender ikiwamo ujenzi wa Nyerere Hydropower inayojengwa na Arab Contractors ya Egypt ili kupata kitu kizuri mezani.

Kama aliweza ku-renegotiate na Barrick mpaka Twiga ikazaliwa na sie kupata 16% ya hisa na Watanzania kuwa kwenye board na executive management team, kwa muono huo, tusimwone alikuwa haoni maslahi ya Tanzania kwenye Bagamoyo port. Ila kwa kuwa kama alikuwa ni "kiuzibe" ashalala; basi wale walio kwenye mamlaka ya kufanya maamuzi kwa niaba yetu mnaweza kulisongesha, ila zingatieni maslahi ya mama Tanzania.

Kiufupi weather tujatenga Bagamoyo port au la, kwa kuwa tushaamua kujenga SGR ya umeme, Tanzania (nikimaanisha serikali) lazima ije na sera rafiki hasa kwa wawekezaji wazawa ambao watazalisha kwa wingi kupitia sekta kama kilimo-biashara; sio kilimo cha kujikimu kikiwa supported na Agri-processing & Manufacturing ili makontena ya processed agro-outputs zipitie kwenye SGR na Port kama mauzo nje ya nchi kwa wingi kuliko makontena ya imports; exports simply bring in forex (inflow ni afya kwa uchumi na kukuza mzunguko), imports simply sends out forex (outflow ikiwa kubwa sio afya kwa uchumi endelevu na uchumi jumuishi). Maana tuna import chupi, leso, mifagio ya buibui, vitambaa vya nguo, mafuta ya kula wakati vitu hivi nchi yetu ina ardhi ya kutosha kuweza kuvizalisha.
Hazina lazima iwe na policy framework ya ku-customize marshall plan export cash crop walau by 70% ziwe domestically proccessed na zipite kwenye SGR na Port kwa wingi, with that tutatengeneza trade surplus na ni afya ku-service deni la ndani au deni la nje

Jumapili njema
 
Sawa maelezo mazuri sana ndugu, bandari ya Bagamoyo ni Muhimu huko mbele ya safari cha msingi tuangalie mashart na tuwe wazalendo kwa maslahi mapana ya nchi
 
Serikali ingejenga bandari ya Bagamoyo kwa kushirikiana na oman na wa China kwa mfumo wa PPP badala ya kuachiwa wao pekee. Bandari na Airport ni malango ya kuingia na kutoka kiusalama serikali lazima iwe na jicho lake hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…