Bandari ya Dar es Salaam ibadilishwe jina iitwe Bandari ya Samia

Bandari ya Dar es Salaam ibadilishwe jina iitwe Bandari ya Samia

Mpaka mseme, yaani mpaka mseme kabisaaaaa

Samia atabaki kuwa rais bora na bora na bora sana
Hembu niambieni angalau rais mmoja tu aliwahi kuruhusu maandamano inchi hii
Wacha rais mmoja hata nusu tu
Kikwete aliruhusu maandamano ya mashehe na waumini wao
 
Huku kwetu gongo la mboto Samia ni kali sana mpaka joto limezidi....Suluhu ina muda mrefu haijanyesha
 
Hata mvua nazo ziitwe Samia.
Kwa vile huyu ‘mama’ yetu amekuwa ndo Rais bora kabisa kuwahi kutokea Tanzania [kama siyo Afrika na hata dunia nzima], mimi naenda mbali zaidi na kutaka awekwe tu kwenye noti.

Mimi napendekeza jina la Bandari ya Dar es Salaam libadilishwe na iitwe Bandari ya Samia/ Port of Samia.

Mama kaleta DP World. Mahela hapo bandarini yameongezeka mpaka pomoni. Mameli ya kutoka Ulaya na kwingineko yanagombania kuja kwenye hii bandari yetu.

Bandari yetu hii sasa imeshika namba ya pili duniani kwa ubora, courtesy of Mama.

Sasa kwa nini tuishie kumuenzi kwenye noti tu?

Tuibadili jina na tuipe jina la Samia.

Na itanoga zaidi pia tutakapoibadilisha jina bahari ya Hindi na kuiita bahari ya Samia.

Na tusiishie hapo. Dodoma nayo tuibadili jina na tuiite Samia.

Na kwa mtaji huo, jina la mji mkuu wetu liwe ni Samia.

Hata mlima Kilimanjaro utapendeza zaidi tukiubadili jina uitwe Mlima Samia!

Mnasemaje wadau..? Tusiwe na wivu. Ungeni mkono hizi juhudi.
Naunga mkono hoja kila kitu kiitwe Samia. Hadi maombi kwa Mungu yaanze na Samia rais wa nchi yetu. Tupo hai kwa ajiri ya Samia.

Wabunge wakitoa hoja, mahakama kabla ya hukuma waanze kumshukuru Samia.
 
Back
Top Bottom