Bandari ya Zanzibar yabinafsishwa kwa kampuni ya kigeni, wazalendo wahoji

Bandari ya Zanzibar yabinafsishwa kwa kampuni ya kigeni, wazalendo wahoji

Chama cha ACT Wazalendo kimehoji juu ya mchakato uliotumika kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuipatia Kampuni kuendesha shughuli za bandari ya Malindi Zanzibar

Katibu wa habari na uenezi ACT Wazalendo Salum Bimani, amehoji hatua hiyo wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kufungua pazia la kuanza kufanyika kwa mikutano 12 Unguja na pemba

Bimani ameitaka serikali ya Zanzibar kueka bayana hatua zilizofanyika za mchakato wa kuipatia kampuni ya Africa Global Logisti kuendesha na kusimamia shughuli za Banadari ya Malindi

Kwani kutoa tender ndiokuuzwa mbona Bara kwetu kuna TICTs
 
Tunaweza kuchukua mfano wa benki ya CRDB. Kilichoifufua ni kuuza baadhi ya hisa kwa mwananchi. Kilichobakia ni historia. Bahati nzuri dkt. Kimei yu hai na akili tumamu ataweza kutielimisha zaidi katika hili. Hata alipokuwa anaondoka mchakato wa kumpata Bw. Majid umeleta matokeo chanya.

Itabidi tukubaliane kuwa huko nje hakuna wajomba wa kutuletea maendeleo, itabidi sisi wenyewe tufunge mkanda. Kampuni ya Emirates ilianza na ndege moja. Kilichofanyika sio kubinafsisha bali alitafutwa CEO kutoka Uingereza na wanasiasa wakajiweka kando na kumpa Uhuru wa kutumia taaluma na uzoefu wake. Sasa Emirates ni kitu kingine. Pengine wakati umefika tupunguze siasa katika masuala ya kitaaluma, tutavuka lakini sio kutegemea wajomba wa nje kwa sababu nao watakuwa na ajenda zao na malengo yao.
Sio kwa ccm hii unataka wao walewapi? Starehe watafanyia mawe?
 
Nyerere alionya sana ubinafsishaji.

Alihofu hata magereza yatabinafsishwa.
Magereza yapo njiani kubinafsishwa. Leo hii unaweza kukodi wafungwa wakufanyie kazi zako. Hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea ubinafishishaji.
 
Mdharau mwiba mguu huota tende.

Bandari ya Malindi imeuzwa kwa kampuni ya Bollore ya Ufaransa! Hussein Mwinyi na Toufiq Turky wamepewa asilimia thelathini ya mkataba, Wafaransa wamebaki na asilimia sabini! Zanzibar iko mnadani!

Au ni kweli?

FB_IMG_1693308946459.jpg
 
Chama cha ACT Wazalendo kimehoji juu ya mchakato uliotumika kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika kuipatia Kampuni kuendesha shughuli za bandari ya Malindi Zanzibar

Katibu wa habari na uenezi ACT Wazalendo Salum Bimani, amehoji hatua hiyo wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika visiwani Zanzibar ikiwa ni sehemu ya kufungua pazia la kuanza kufanyika kwa mikutano 12 Unguja na pemba

Bimani ameitaka serikali ya Zanzibar kueka bayana hatua zilizofanyika za mchakato wa kuipatia kampuni ya Africa Global Logisti kuendesha na kusimamia shughuli za Banadari ya Malindi

Tunasubiri Jusa atasemaje
 
Back
Top Bottom