Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,430
BANDARI YAHUDUMIA TANI MILIONI 32 KUTOKA TANI MILIONI 18
Kufuatia maboresho, Bandari ya Dar es Salaam imehudumia tani milioni 32 kutoka milioni 18 mwaka 2021.
Hayo yameelezwa Agosti 26, 2025 wakati wa kikao cha wadau wa Kamati ya Maboresho ya Bandari, kilichoendeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Profesa Godius Kahyarara.
Aidha, imebainika kuwa gharama za uendeshaji katika bandari hiyo kwa upande wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), zimepungua kutoka kiasi cha Sh. Bilioni 652.83 kwa mwaka 2023/24 hadi kufikia bilioni 268.73 mwaka 2024/2025.
Taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao hicho imebaini kuwa uwekezaji bandarini humo umeleta mitambo ya kisasa.
"Ni usimikaji mitambo minane inayotambulika kama 'Rubber Tyred Gantry Crane-RTG' katika Gati Na. 1 la makasha la Bandari ya Dar es Salaam.
"Kabla ya kufanyika kwa uwekezaji huu, TPA ilikuwa na mitambo miwili tu ya aina hii wakati mahitaji halisi yalikuwa ni mitambo ya aina hii isiyopungua 10 kwa wakati mmoja," amesema.
Hatua nyingine ni ununuzi wa mitambo miwili aina ya 'Ship to Shore Gantry Cranes-SSG' kutoka TPA ambayo ilinunuliwa kwa ajili ya kutumika katika Kitengo Na. 1 cha makasha.
"Kadhalika kuna 'terminal tractors' ishirini (20) ambazo hutumika katika kuhamisha na kusafirisha shehena kutoka eneo moja la bandari kwenda eneo jingine na 'trailers' 31 ambazo hutumika katika kubeba shehena za aina mbalimbali.