Bandari za Tanganyika hazijauzwa wala kukodishwa kwa waarabu wa Dubai bali zote wamepewa bure!

Bandari za Tanganyika hazijauzwa wala kukodishwa kwa waarabu wa Dubai bali zote wamepewa bure!

Aliyefikiria swala muungano alikosea sana sijui aliwaza nini mtu atoke huko Zanzibar aje atutawale huku mbaya zaidi bunge nalo ni dhaifu
 
Inauma
Screenshot_20230615-122154_Keep Notes.jpg
 
Mkuu ni afadhali alijenga nchi japo upande wa demokrasia hakuwa vizuri but maeneo mengi alikua vizuri.

Huwezi pata kiongozi perfect kila eneo.
Hao wanaoauza Nchi Wote Ndiye Aliwapeleka
Bungeni. Hakuwa na Maono zaidi ya Ubabe
 
Tz ilipata kiongozi mzuri mkawa mnamtusi humu,ukitoa mapungufu kidogo tu alikuwa anaipenda nchi yake.
Sasa mtajua hamjui.
Lile nalo ni jinga sema ukali wake ulilifanya lionekane bora
 
Nimesikitika sana kusikia malumbano ya watu mbalimbali kuhusu suala la kuuzwa dhidi ya kukodishwa kwa bandari zote za mwambao wa bahari ya Hindi upande wa Tanzania bara kwenda kwa waarabu wa Dubai (DP world).

Baada ya kupitia kwa kina, kipengele kwa kipengele, kusikiliza maoni tofauti tofauti ya watu wenye uelewa na weredi kuhusu mikataba na sheria, nimegundua wazi bila shaka yoyote kuwa, Bandari zote za mwambao wa bahari ya Hindi upande wa Tanzania bara amepewa BURE muarabu wa Dubai. Narudia kusema muarabu wa Dubai amepewa BURE. Hajauziwa wala kukodishiwa. Sababu muhimu ni hizi hapa.

1. Hakuna mahali popote kwenye mkataba panaposema ameuziwa bandari au kueleza bei ya manunuzi ama kiasi kilicholipwa ili muarabu apewe bandari. Mkataba indirectly unasema Muarabu wa Dubai amepewa milele ili apaendeleze na hatupaswi kumfanya chochote akishindwa kupaendeleza!

2. Hakuna mahali popote kwenye mkataba panapotaja ni lini au namna gani bandari yetu tutarejeshewa tena. Ukodishaji wowote wa jambo unabanwa na mambo mawili tu. Mosi mipaka ya muda (ni lazima useme ukomo wa muda wa kukodisha) na pili Urejeshaji ya kile kilichokodishwa (ni vipi mkodishaji atarudishiwa mali yake aliyoikodisha). Kwenye mkataba huu hakuna popote panaposema hayo. Pako kimya kabisa.

Note
Tafsiri nyingine ya kiujumla jumla ya BURE ni; Uuzwaji wa kitu cha thamani kwa bei ndogo sana isiyolingana na bei ya soko au uuzwaji wa tunu (kitu chenye thamani kubwa kijamii isiyoweza kubadilika na chenye kuwa na sifa ya kurithiwa na vizazi vyote vijavyo milele)

Pia kukodisha kitu kwa mtu mwingine kwa kipindi cha muda mrefu unaopitiliza muda wa matarajio ya wewe au kizazi chako cha sasa kuendelea kuwepo hai (kiutendaji) duniani maana yake ni kubadilisha umiliki kutoka kwako kwenda kwa yule unayemkodishia. Ukodishaji wowote unaozidi miaka 20 huo ni umilikishaji.
Mkuu ulihitimu chuo gani katika hiyo kozi yako ya kufitinisha?
 
Nae aliwahi kutupeleka utumwani Dubai?
Alitupeleka utumwani kwao Isimani kwao alivyokuwa anaiba ardhi za watu na kujimilikisha ni jambazi wa mali za watu tusidanganyane ni nyangau kama manyangau mengine
 
Mkuu hapo nakataa
Jpm alikuwa hajui concepts za uchumi mbeleni tulikuwa tunaendelea kukwama.Huwezi kutangaza vita live na wazungu wenye remote remote ya uchumi wetu na afya zetu.
 
Wakati mnaendesha wenyewe mmepata faida gani?
Hakuna, na ndio maana nasema ni aibu kwamba tunashindwa kuendesha taasisi zetu hadi leo, je tunataka kuendelea kutawaliwa na wageni?
 
Back
Top Bottom