Bangi Meru yawaponza OCD, OCCID, DSO. Rais Magufuli awaondoa | Amthibitisha James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya

Bangi Meru yawaponza OCD, OCCID, DSO. Rais Magufuli awaondoa | Amthibitisha James Kaji kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya

Tukilindana umma utanufaika nini? Kila mtendaji afanye kazi angalau kwa wajibu wake. Haina maana ya kuwa mtendaji na eneo lako la kazi limetawaliwa na madhaifu. Ni aidha hautoshi (incapable) ama hauna msukumo wa kutosha. Sasa atakayekutonya hapo si atakuwa adui wa maendeleo?
Rushwa ndo haivumilika lakini suala dogo la kiutendaji ndo mpaka wakubwa wapate taarifa???? Kuna kujisahau au kuzidiwa ujanja inabidi tusaidiane
 
Bangi haijawahi mteketeza mtu labda iwe imechanganywa na vitu vya kijinga. Ligeuzwe kuwa zao la kibishara
Hao watakuwa siyo ccm ndo maana! Uza bangi uwe Mwana ccm, haufuatwi. Wengine wanaweka tu bendera ya ccm mambo shwari kabisa.

Hao waliotumbuliwa na bangusilo tu.😀
 
... kwani kuna Arumeru na Meru? Formally Arumeru nowadays Meru.
Mbona arumeru makao yako ngaramtoni? Na meru ndio hapo usariva na arusha ni pale philips na manispaa ni mjini kati. Au nimekosea.
 
Wengi wamesahau wajibu wao wapo busy na wapinzani pumbavu kabisa.
 
Rais Magufuli wakati wa hafla ya kuwaapisha viongozi wateule amewaagiza wakuu wa vyombo vya usalama nchini kuwaondoa Mkuu wa Polisi wilaya ya Meru na Mkuu wa Usalama wa Wilaya Meru kuondolewa maeneo yao ya kazi kutokana na kukithiri kwa zao la bangi bila kuchukuliwa hatua madhubuti.

Rais Magufuli amesema haya...

“Nimekuona jana au juzi ulikagua kijiji kwa kijiji na kukuta gunia za Bangi, sasa IGP nataka mkuu wa Polisi wa Meru aondolewe, DSO wa Meru aondoke, maana yake hawakutimiza wajibu wao, haiwezekani mtu atoke Dar aende akakamate Bangi Meru wakati wao wapo”

OCCID wote watoke, ikiwezekana washushwe cheo maana hatuwezi kwenda kwenye utaratibu huo. Na wewe wa Kitengo cha Madawa nakuthibitisha leo


Pia, Rais Magufuli amemthibitisha Kaimu Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, James Kaji, kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka hiyo, leo Julai 06, 2020.

Huyu Kamishna wa Madawa ya Kulevya siwezi nikamuapisha hapahapa?, tengenezeni kiapo haraka mkimaliza nimuapishe sitaki kurudi tena hapa

Rais Magufuli akimuapisha James Wilbert kuwa Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya nchini.
Shida ya polisi Arusha group kubwa hupangwa barabarani kukusanya pesa kwenye magari
Maaskari wa operations ni wachache sana. Ukiwa na shida ukienda kituoni unaambiwa askari hakuna. Lakini brabarani utakutana nao kila baada ya mita mia.
Nadhani hiki jambo limemshinda IGP
Ni muda muafaka sasa Mh Rais aliingilie ili usumbufu barabarani upungue na nguvu kubwa ielekezwe kwenye matukio kama hayo ya bangi na ujambazi.
 
Pongezi kwa kamishna mpya Bwn. Kaji.
 
Hata DC naye angepigwa chini yeye ana kazi ya kushabikia Yanga huku watu wanateketea kwa bangi.


Na ndiye Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya, kama mtu kutoka Dar amekwenda na kuyaona hayo maana yake ni kwamba wilaya haikuwa salama hata kidogo
 
Waanaambiwa wawe bize na kazi za kuisaidia CCM kubaki madarakani, huku majukumu yao ya kimsingi wakikosa muda wakuyashughulikia.

Mwishowe anawaambia wameshindwa kazi!!
Ndo.apo sasa kakangu,mnyonge mnyongeni ila haki yake apewe,ila nao wanazid mno kuutesa UPINZANI
 
Chadema watapinga na kusema Lisu tu ndiyo shujaa wa bangi
Wewe Dada haiyumkini unaishia buza kwa lulenge kwani tabia yako inaakisi maeneo hayo! Lissu atarudi tu na atagombea hata Kama hutaki! Kama vipi kunywa sumu ufe itapendeza!
 
hivi wana CCM wenzangu mbona mna nye-ge na Chadema kiasi hichi? aibu kwa chama!
Bora umewaona! Hao ndio wanafiki ninaowasema kila siku kuwa wamejazana ccm kwa maslahi yao yasiyosaidia chama na kimsingi wanaipigia promo cdm ili ijulikane zaidi!
 
Kama DSO ( District Security Officer ) au Afisa Usalama wa Taifa wa Wilaya ya Arumeru ametumbuliwa Leo na Bosi wake Mkuu Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli je, hii haitoshi labda kuwa ni wake up call kwamba huenda kwa sasa Idarani huko kuna Watumishi wasio na maadili ambao wanaweza siku moja kuja Kuigharimu hii nchi?

Sasa kama tu DSO anakuwa na Mapungufu haya Kiutendaji vipi kwa hawa RSO's na hata Mkurugenzi Mkuu na Makamu wake? Wajitathmini upesi.
 
Back
Top Bottom