Bangi na pombe Kali ni hatari nimerudi mtaani naona vijana wamezeeka ghafla

Bangi na pombe Kali ni hatari nimerudi mtaani naona vijana wamezeeka ghafla

Sio kweli mzee watu wamezeeka ghafla tena ni kundi Hilo tu la bangi na pombe Kali yaani majanja wamezeeka ghafla aisee ccm
Hawafai tena UVCCM labda jumuia ya wazazi 😁😁
 
Inategemeana na maisha ya mtu, ukienda mitaa ya wenye uwezo kama masaki wapo wavuta bange na wanywa pombe kali lakini sura zipo kawaida, Hii ni kwasababu hawana stress za maisha hasa kiuchumi, milo mitatu ya uhakika ipo, umeme na amaji vipo, pocket money elf ipo kila siku hata kama hana ajira

Ila nenda maeneo mengine hasa uswazi, vijana wana stress nyingi sana, kijana kakamua hadi degree lakini hana ajira, kila siku akirudi kwao ni kelele za unahama lini, umeleta nini, n.k. muda huo huo kashamjaza uja uzito binti wa mtaani, stress zinazidi atahudumia vipi mtoto, hapo ukinywa pombe na kuvuta bange unazeeka haraka sana
 
Ni kweli kabisa , mimi marafiki zangu wavuta bange na madogo wavuta bange wa mtaani sura zao zinatisha , zimekomaa na kuwa kama wazee wakati vijana wadogo.

Nadhani inachangia na kiwango Cha uvutaji na haki ya maisha . Mtu akiwa Mshua mo uhakika , hafanyi kazi ngumu na anavuta kwa kiasi anakuwa kawaida tu.
Kabisa Kuna mmoja anaonekana kawaida yeye akija kijiweni anachukua kete anaenda kuvuta kwao ni wakishua. Yaani hataki kukaa sana ni gwala stori mbili tatu anatembea
 
Waambie wazingatie msosi wa kutosha na muda mwingi kupumzika basi kama vinazeesha Sugu angekuwa Kibabu

Naunga mkono hoja...

Mara nyingi naona nyuzi huku kuchanganya pombe Kali na vinywaji nishati (energy drinks) ni msala ila nikimcheck moto chini Toka kitamboo na yupo gado tu analinda himaya.
 
Inategemeana na maisha ya mtu, ukienda mitaa ya wenye uwezo kama masaki wapo wavuta bange na wanywa pombe kali lakini sura zipo kawaida, Hii ni kwasababu hawana stress za maisha hasa kiuchumi, milo mitatu ya uhakika ipo, umeme na amaji vipo, pocket money elf ipo kila siku hata kama hana ajira

Ila nenda maeneo mengine hasa uswazi, vijana wana stress nyingi sana, kijana kakamua hadi degree lakini hana ajira, kila siku akirudi kwao ni kelele za unahama lini, umeleta nini, n.k. muda huo huo kashamjaza uja uzito binti wa mtaani, stress zinazidi atahudumia vipi mtoto, hapo ukinywa pombe na kuvuta bange unazeeka haraka sana
Aisee sio poa mkuu kijana wa miaka 17 usoni kama mzee wa miaka 40
 
Bangi haizeeshi mkuu,maisha yao magumu tu...
itoe bangi kwenye maisha yao halafu angalia wanabaki na nini
 
Hivyo wanavyovitumia nasisi tunavitumia pia ndio nimekwambia Wana matatizo yao mengine.
Unakuta hawapati chakula kama inavyostahili,
Hawapati maji ya kutosha,
Wanakua na msongo wa mawazo
Uzinzi uliokithikiri
Hawapati muda wa kupumzika
Hawana majukumu ya kuwafanya wawe busy.
Kwaiyo bangi na pombe Kali isisingiziwe
Sahihi kbsa
 
Kuna siku usingizi ulikata nikatoka nje kufika namkuta jirani yangu naye katoka nje usingizi umekata akaita boda anamfahamu tukaenda sehemu kupoteza muda, huyo boda alikuwa ananuka harufu ya bangi na pombe kali nashukuru tulifika salama.
 
Sasa mletewa pombe 2000 kisungura ukipiga chupa mbili vidogo kwisha habari

Ova
 
Back
Top Bottom