Bar kutumia wanawake maids kama kivutio cha biashara ni sawa na biashara ya danguro?

Sex sells

Na haipo tu kwenye mabar

Kwenye entertainment business bila msanii wa kike kuvaa kimitego haiendi na imeingia hadi kwa DJs, video vixens na mara nyingine hadi actresses

Kwenye kampuni nyingi, mabinti wa ushering, promotions, customer service au sales. Muonekano huzingatiwa na nguo flani nadhifu

Bado hujaongelea wahudumu wa migahawa, mama ntilie etc

Kiufupi wanawake washaonekana ni wa ngono kwa hiyo kada nyingi zipo hivyo kutokana na mindset za watanzania wengi. Sio issue ya career ila mtazamo wa watu
Kwa sasa hadi wahudumu wa SGR wameingizwa kwenye huo mfumo.
 
Huu mtindo wa Bar nyingi kuwatumia wanawake/ mabinti barmaids kwa kuwavalisha mavazi ya aina fulani ili wawe kama chambo/ kivutio cha biashara zao kingono una tofauti gani na uendeshaji madanguro (brothels)?

Nafikiri umefika wakati sasa serikali itambue rasmi biashara za danguro na itofautishe na bar.
Ni kweli. Ila wenye mamlaka ndiyo wamiliki wa bar kubwa zote mjini.
Kamanda Siro RC kigoma ni mfano hai.
Nani atamsimia nani?
 
Wasikamatwe, waelekezwe tu tofauti ya bar na night club
 
Huu mtindo wa Bar nyingi kuwatumia wanawake/ mabinti barmaids kwa kuwavalisha mavazi ya aina fulani ili wawe kama chambo/ kivutio cha biashara zao kingono una tofauti gani na uendeshaji madanguro (brothels)?

Nafikiri umefika wakati sasa serikali itambue rasmi biashara za danguro na itofautishe na bar.
Comrade, fungua Bar yako ya mfano halafu wavishe wahudumu wako wote magauni ya spesheli kama yale ya Ndalichako uone kama utapata wateja.
 
Kwenye muziki, movies na promotions naweza kuelewa kwa sababu pia ni rahisi kufanya uamuzi wako binafsi, sasa bar ndio sehemu ya kukutana kwa Tanzania na wakati mwingine mtu anaweza kwenda hata na mke au familia. Kuna umuhimu wa kutenganisha bar na strip club.
Unakwenda na mke/familia bar kufanya nini? Unachokitafuta ipo siku utakipata. Unaenda washroom, wahuni wanachukua namba faster!

Na wakigundua unakabia juu, wanamtuma mhudumu huyo huyo mwenye mavazi ya kutatanisha kuchukua namba ya mke wako na ukiwa hapo hapo umezubaa.
 
Kumbe Bar za bongo ni wahuni na wakora watupu! Lkn hata wakichukua namba ya wife wanapoteza muda tu.
 
Comrade, fungua Bar yako ya mfano halafu wavishe wahudumu wako wote magauni ya spesheli kama yale ya Ndalichako uone kama utapata wateja.
Kwa hiyo Bar za bongo watu wana wanaenda kufuata wanawake tu!
 
Huu mtindo wa Bar nyingi kuwatumia wanawake/ mabinti barmaids kwa kuwavalisha mavazi ya aina fulani ili wawe kama chambo/ kivutio cha biashara zao kingono una tofauti gani na uendeshaji madanguro (brothels)?

Nafikiri umefika wakati sasa serikali itambue rasmi biashara za danguro na itofautishe na bar.
Ni wazi kuwa baadhi ya wamiliki wa baa wanavuka mpaka wa uhudumu wa kawaida na kuingia kwenye unyonyaji wa kingono kibiashara. Hatua ya sasa inayohitajika zaidi kisheria ni mamlaka zinazotoa leseni kusimamia maadili ya kazi na usalama wa wafanyakazi wa kike maofisini na kwenye baa, ili kuhakikisha utu wao hauuzwi kama sehemu ya bidhaa.
 
Jumamosi moja Mkipata nafasi nendeni tips pale Mikocheni mida ya usiku
 
Ni wazi kuwa baadhi ya wamiliki wa baa wanavuka mpaka wa uhudumu wa kawaida na kuingia kwenye unyonyaji wa kingono kibiashara. Hatua ya sasa inayohitajika zaidi kisheria ni mamlaka zinazotoa leseni kusimamia maadili ya kazi na usalama wa wafanyakazi wa kike maofisini na kwenye baa, ili kuhakikisha utu wao hauuzwi kama sehemu ya bidhaa.
Sahihi, Sheria itungwe kuzuia wamiliki bar kupangia wahudumu sare za mavazi isipokuwa rangi tu.
 
Kwa kweli binti anayeenda kutafuta riziki ya halali ya kuhudumia wanywaji wa bia na vinywaji vingine anastahili kulindwa na sheria ili asilazimike "kuuza mvuto wake" ili kulinda kibarua chake.
 
Back
Top Bottom