Bar kutumia wanawake maids kama kivutio cha biashara ni sawa na biashara ya danguro?

Kwa sasa hadi wahudumu wa SGR wameingizwa kwenye huo mfumo.
 
Ni kweli. Ila wenye mamlaka ndiyo wamiliki wa bar kubwa zote mjini.
Kamanda Siro RC kigoma ni mfano hai.
Nani atamsimia nani?
 
Ni kweli. Ila wenye mamlaka ndiyo wamiliki wa bar kubwa zote mjini.
Kamanda Siro RC kigoma ni mfano hai.
Nani atamsimia nani?
Wasikamatwe, waelekezwe tu tofauti ya bar na night club
 
Comrade, fungua Bar yako ya mfano halafu wavishe wahudumu wako wote magauni ya spesheli kama yale ya Ndalichako uone kama utapata wateja.
 
Unakwenda na mke/familia bar kufanya nini? Unachokitafuta ipo siku utakipata. Unaenda washroom, wahuni wanachukua namba faster!

Na wakigundua unakabia juu, wanamtuma mhudumu huyo huyo mwenye mavazi ya kutatanisha kuchukua namba ya mke wako na ukiwa hapo hapo umezubaa.
 
Kumbe Bar za bongo ni wahuni na wakora watupu! Lkn hata wakichukua namba ya wife wanapoteza muda tu.
 
Comrade, fungua Bar yako ya mfano halafu wavishe wahudumu wako wote magauni ya spesheli kama yale ya Ndalichako uone kama utapata wateja.
Kwa hiyo Bar za bongo watu wana wanaenda kufuata wanawake tu!
 
Ni wazi kuwa baadhi ya wamiliki wa baa wanavuka mpaka wa uhudumu wa kawaida na kuingia kwenye unyonyaji wa kingono kibiashara. Hatua ya sasa inayohitajika zaidi kisheria ni mamlaka zinazotoa leseni kusimamia maadili ya kazi na usalama wa wafanyakazi wa kike maofisini na kwenye baa, ili kuhakikisha utu wao hauuzwi kama sehemu ya bidhaa.
 
Jumamosi moja Mkipata nafasi nendeni tips pale Mikocheni mida ya usiku
 
Sahihi, Sheria itungwe kuzuia wamiliki bar kupangia wahudumu sare za mavazi isipokuwa rangi tu.
 
Sahihi, Sheria itungwe kuzuia wamiliki bar kupangia wahudumu sare za mavazi isipokuwa rangi tu.
Kwa kweli binti anayeenda kutafuta riziki ya halali ya kuhudumia wanywaji wa bia na vinywaji vingine anastahili kulindwa na sheria ili asilazimike "kuuza mvuto wake" ili kulinda kibarua chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…