Bar Maids wa Kisuma Bar Magomeni njaa kali

Bar Maids wa Kisuma Bar Magomeni njaa kali

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Bar Maid wengi sio wameingia katika kazi hii kwa kupenda hii ni kazi kama kazi nyingine, nina mifano mingi sana marafiki na ndugu zetu wamepata wenzao kupitia hawa Bar Maid.

Siku mbili hizi nilibahatika kwenda Magomeni Usalama pale kuna wauzaji wa magari ya mkononi. Nikatia timu Bar inaitwa Kisuma. Pale kuna wahudumu wamejaliwa sana wana mizigo haswa. Nikaagizia chakula mimi situmii kilaji. Nikawa nimekaa na jamaa wawili akaja mhudumu akatusikiliza.

Mimi nikaagizia changu nao jamaa wakaagizia chao. Wakampa ofa bibie mhudumu awajoin wakamuuliza unatumia kinywaji gani akasema sijui Windhoek akaambiwa chukua mbili. Alivyotoka kwenda kuhudumia meza nyingine nikasikia njemba zinalia huyu dada sio kabisa sasa hizi bia mbili ni 7000 kwani asingekunywa bia ya kawaida na akabakisha pesa hata ya kuwekeza ndani.

Looh nikajiuliza mhudumu huyu mbona hana akili unachoma 7000 wakati hata angewaambia ninunulie chakula nitakula baadae.

Nikasema acha niangalie meza zingine walizokaa wahudumu unakutana na Windhoek na zile sijui Pri nini sijui ukiuliza bei ni 3500 Bar Maid unachoma pesa hiyo kwa ushamba wa kuiga vya mjini ukitoka hapo hauna hata mia ya mihogo ama utakuta wanalala gheto.

Kisuma Bar ukweli mna wadada wadada ambao hata shekhe kipozeo udenda unamtoka ila badilikeni kunywa maji ya Ilala utaweza hata kupewa chenji.
 
Wewe ulichoma bei gani?
Sasa wewe unaumia nini? Unadhan ni watoto kama wewe unakunywa novida Bar
Kwanza hata ningekuwa nakunywa nisingeweza kumnunulia bia mtu yupo kazini. Kwa akili zako wote wasiokunywa ni watoto basi uenda kati ya wazazi wako wawili kuna mtoto ama wote watoto.
 
Mkuu, ulichosema ni kweli! Nami, nilishuhudia baa moja, Mwanza mjini. Nikajiuliza, hivi hao wahudumu, kwa fedha yao, wanaweza kununua kinywaji cha bei ghali hivyo?

Kwa nini kinywaji cha kununuliwa, wanachagua cha bei kubwa hivyo? Kufuatilia, nikamuona mmoja, anajaza soda ya Novida kwenye chupa ya Savana!

Hivyo, hata huko, sina shaka hawanywi hizo pombe, ila hao walipaji wanalipia kwa hiyo bei ghali, cha juu wanachukua. Pia, hao wahudumu huwa wana umoja sana, pindi litokeapo deal la namna hiyo!
 
Mkuu, ulichosema ni kweli! Nami, nilishuhudia baa moja, Mwanza mjini. Nikajiuliza, hivi hao wahudumu, kwa fedha yao, wanaweza kununua kinywaji cha bei ghali hivyo? Kwa nini kinywaji cha kununuliwa, wanachagua cha bei kubwa hivyo? Kufuatilia, nikamuona mmoja, anajaza soda ya Novida kwenye chupa ya Savana!
Hivyo, hata huko, sina shaka hawanywi hizo pombe, ila hao walipaji wanalipia kwa hiyo bei ghali, cha juu wanachukua. Pia, hao wahudumu huwa wana umoja sana, pindi litokeapo deal la namna hiyo!
Hapa kuna watu wanaona nimeleta ujinga hao jamaa nimekaa nao walikuwa wanalalamika sana.

Na hata hawa wahudumu wa Kisuma akili hakuna ama ni mpango mkakati wa wamiliki wa Bar kutaka hizi pombe za bei zitoke.

Najua Bar Maid ambao walikuwa wanahudumu Rose Garden, Mango Garden na Jackys wamejenga na ilikuwa ni nadra sana kuwakuta wanalewa lakini Kisuma Bar Maid anapiga chupa kama mteja.
 
Kuna siku mmoja akinishobokea eti na yey anata nimnunulie windhoek Nikamwambia hpn Kama Ni safar au Serengeti hata kumi nitakunulia ila hyo hapana.

Akasema akaniomba nimpe hyo elf tatu za bia mbili ili ajiongeze anunue bia anayopenda yey pia nikamwambia hnp

Mm huwa namnunulia demu bia za ndani tu na simpi kash

Siri iko kwamb mameneja ndio wanawalazimisha kunjwa hizo bia ili waweke standard huu ujinga upo dagadaga na bar kibao tu
Sitafanya hyo buahiara Kam atatumia Safari namnunulia syo hz
 
Nakumbuka siku moja nilienda kiwanja kimoja mjini mwanza nikiwa na dogo langu(msela) akiwa kavaa kawaida sana na anakunywa maji.

Kuna bar maid alimuelewa sana akamuita na kumuomba namba yule bar maid akamjibu kwa jeuri sana kwamba ukitaka kuongea na mimi ninunulie kinywaji akanunuliwa Hennessy (pale wanauza 300k Hennessy kubwa) alafu akamwambia usikae na mimi sijapenda perfume yako nipe namba ukakae sehem tofauti na mimi then nitakutafuta, dogo hakumtafuta wala nini kakausha tu.

Kila muda yule bar maid anakuja kuuliza mbona hunipigii baby dogo anamchora tu.
 
Nakumbuka siku moja nilienda kiwanja kimoja mjini mwanza nikiwa na dogo langu(msela) akiwa kavaa kawaida sana na anakunywa maji. Kuna bar maid alimuelewa sana akamuita na kumuomba namba yule bar maid akamjibu kwa jeuri sana kwamba ukitaka kuongea na mimi ninunulie kinywaji akanunuliwa hennessy(pale wanauza 300k Hennessy kubwa) alafu akamwambia usikae na mimi sijapenda perfume yako nipe namba ukakae sehem tofauti na mimi then nitakutafuta, dogo hakumtafuta wala nini kakausha tu. Kila muda yule bar maid anakuja kuuliza mbona hunipigii baby dogo anamchora tu.
Oya Moderator nini hizi?
 
Nakumbuka siku moja nilienda kiwanja kimoja mjini mwanza nikiwa na dogo langu(msela) akiwa kavaa kawaida sana na anakunywa maji. Kuna bar maid alimuelewa sana akamuita na kumuomba namba yule bar maid akamjibu kwa jeuri sana kwamba ukitaka kuongea na mimi ninunulie kinywaji akanunuliwa hennessy(pale wanauza 300k Hennessy kubwa) alafu akamwambia usikae na mimi sijapenda perfume yako nipe namba ukakae sehem tofauti na mimi then nitakutafuta, dogo hakumtafuta wala nini kakausha tu. Kila muda yule bar maid anakuja kuuliza mbona hunipigii baby dogo anamchora tu.

Cha ajabu nini hapo!.

Hiyo Hennessy ya laki tatu muhudumu kachukua 270 yake safi kaunta.

Nyie wenye kiburi cha fedha ndio wanawapenda!

Kwa hiyo dogo anamkomoa mhudumu!

Hahahahah.
 
Back
Top Bottom