Bar zilizofungiwa zatakiwa kulipa Faini Milioni Tano 5M kila moja ili ziruhisiwe kufanya biashara

Kuna viwanda na migodi kibao inachafua mazingira ila wanafungia bar kisa mziki.
Umeona eeh, yaani athari za kimazingira za viwanda vinavyotirisha sumu haiwezi kuwa sawa na athari za mziki, afterall mziki siyo kelele bali ni burudani.
 
Mbona hii imeanza kuwa kama ujambazi sasa, kukbe ishu sio kelele, ishu ni walikataa kuwapa hiyo milioni 5, mbona watu wakijitahidi kupambana kihalali kabisa mnawawekea vikwazo?!
 
Kwanini wapige mziki maeneo ya makazi ya watu kwa sauti ya ajabu ajabu?! Haiwezekani kuuza bar mziki ukiwa wa kawaida tu?!
1.)Sasa wakajenge bar kwenye makazi ya wanyama halafu Simba ndio wanywe hizo bia?
2.) Kama hakuna mziki si bora ninyee bia sebuleni kwangu, nimefuata nini bar kama hakuna amsha amsha?
 
Ki ufupi biashara ni changa moto, fikiria bar ya kawaida kupata faifa million Tano unaikusanya kwa kipindi gani? Bahadhi ya watendakazi wa nchi hii ni makatili, mamlaka zinapaswa kuelekeza na kushauri,

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
 
Mkuregenzi WA NEMC amezipa siku Kumi na NNE waliofungiwa bar kulipa Faini ya shillingi milioni tano la sivyo watazifutia lesini.

Mtumishi huyo WA umma ameyasema hayo Leo wakati akitoa taarifa Kwa vyombo vya habari. Hali hii inazidi kuonyesha namna ilivyo ngumu kufanya biashara Tanzania na ilivyo ngumu Kwa sekta binafsi kutoboa.

Wakati akitoa kauli hii hakuna sehemu alipoweza kufafanua
1. Waajiriwa katika bar hizi wataishi vipi?

2. Mapato ya bar husika Kwa mwezi ni kiasi gani?

3. Milioni tano akiambiwa yeye alipe anao uwezo wa kulipa?

4. Anapopanga kuzifutia leseni Kodi inayopotea itapatikana Kwa njia gani

5. Waliolipa Kodi ya biashara kwenye hizo bar mfano wenye leseni ya chakula ndani ya bar hizo ambao NI tofauti na mmiliki WA bar anaathirika vipi?

6. Serikali ikigikishwa mahamani na kudaiwa fidia Kwa hasara alizosababisha atalipa yeye?

7. Wakati wa ufungaji WA bar husika watu wa NEMC awakuweza kukusanya ushahidi WA makosa yaliyotendwa, je serikali ikitakiwa kuthibitisha hayo ataweza kulisaidia Taifa?

8. Nani aliyetoa leseni ya hizi biashara? Nini mtizamo WA taasisi nyingine?

Haya na mengine yalipaswa kutangulia faini lakini Kwa kuwa mfumo uliopo unatamani wanaojitegemea wasifanikiwe na wanaoiba kama walivyotajwa kwenye ripoti ya CAG wafanikiwe basi ..........

Matokeo yake Kwa mambo haya hakuna mchina wala muhindi wala hata mbongo serious ataweka pesa zake Tanzania ; wote watazitorosha kwenda kuzihifadhi nje.

Taifa langu Tanzania mnavyowatesa Watanzania sidhani kama mnaweza kuzitesa biashara za mabeberu hivi.......

Ikivuma Sana inakaribia kupasuka
Sahzi kelele za miziki zimepungua kwa asilimia kubwa Sana maana tulikuwa hatulali .NEMC ishikilie hapohapo
 
Ki ufupi biashara ni changa moto, fikiria bar ya kawaida kupata faifa million Tano unaikusanya kwa kipindi gani? Bahadhi ya watendakazi wa nchi hii ni makatili, mamlaka zinapaswa kuelekeza na kushauri,

Sent from my Infinix X688C using JamiiForums mobile app
Labda km hujaijua taarifa kamili ni kwmb kuna faini ya 5M kwa wakaidi wa onyo la kupunguza sauti na 2M kwa wapya wa game ,ko me nadhan me sahihi kwa iyo faini kwa mkaidi
 
Mkuregenzi WA NEMC amezipa siku Kumi na NNE waliofungiwa bar kulipa Faini ya shillingi milioni tano la sivyo watazifutia lesini.

Mtumishi huyo WA umma ameyasema hayo Leo wakati akitoa taarifa Kwa vyombo vya habari. Hali hii inazidi kuonyesha namna ilivyo ngumu kufanya biashara Tanzania na ilivyo ngumu Kwa sekta binafsi kutoboa.

Wakati akitoa kauli hii hakuna sehemu alipoweza kufafanua
1. Waajiriwa katika bar hizi wataishi vipi?

2. Mapato ya bar husika Kwa mwezi ni kiasi gani?

3. Milioni tano akiambiwa yeye alipe anao uwezo wa kulipa?

4. Anapopanga kuzifutia leseni Kodi inayopotea itapatikana Kwa njia gani

5. Waliolipa Kodi ya biashara kwenye hizo bar mfano wenye leseni ya chakula ndani ya bar hizo ambao NI tofauti na mmiliki WA bar anaathirika vipi?

6. Serikali ikigikishwa mahamani na kudaiwa fidia Kwa hasara alizosababisha atalipa yeye?

7. Wakati wa ufungaji WA bar husika watu wa NEMC awakuweza kukusanya ushahidi WA makosa yaliyotendwa, je serikali ikitakiwa kuthibitisha hayo ataweza kulisaidia Taifa?

8. Nani aliyetoa leseni ya hizi biashara? Nini mtizamo WA taasisi nyingine?

Haya na mengine yalipaswa kutangulia faini lakini Kwa kuwa mfumo uliopo unatamani wanaojitegemea wasifanikiwe na wanaoiba kama walivyotajwa kwenye ripoti ya CAG wafanikiwe basi ..........

Matokeo yake Kwa mambo haya hakuna mchina wala muhindi wala hata mbongo serious ataweka pesa zake Tanzania ; wote watazitorosha kwenda kuzihifadhi nje.

Taifa langu Tanzania mnavyowatesa Watanzania sidhani kama mnaweza kuzitesa biashara za mabeberu hivi.......

Ikivuma Sana inakaribia kupasuka
Wacha kuongea pumba wewe lazima wafuate sheria watu hawawezi pumzika majumbani mwao kisa miziki,hata makanisa ya kirokole nayo ya pigwe faidi
 
Back
Top Bottom