Bar zinavyochipuka ukanda wa Mbezi Beach

Bila kuzingatia hili tutafika mahali utulivu utakoseakana kabisa majumbani familia zitayumba na watoto wa shule kupoteza mwelelekeo kimasomo
Wewe umenielewa vizuri mkuu
 
Niliagiza bucket Juliana...nilikuwa nimekaa karibu na vijana kadhaa karibu ,Ile naangalia pembeni si wakachomoa vinywaji......kweli vijana wa uswahili wanaharibu Sana image ya hizi bar siku hizi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ukitaka sehemu ya utulivu walau uingie pale Kibo Complex juu/club 71.
Hakuna changanyikeni.
 
Wajanja sahv wanakaa kwenye viduka kwa mangi,au kwenye vi grocery/pub zikizotulia
Siyo unakaa sehemu mnashindwa hata kuyajenga

Ova

Upo sahihi.. wajanja sio watu wa kwenda sehemu zenye vurugu nyingii.. watu wengi wauza sura..

Kwa mangii mitaani kuna watu wengi sana wenye maisha yao mazuri wanakula bia huku wanabadilishana mawazo kila siku baada ya kazi
 
Hakika mkuu, hizi bar hasa Juliana inakusanya takataka kutoka kila kona ya Dar kwa sasa
 
Mbezi Beach ilishakongoroka kitambo tu mbona.

Kwa sisi ambao tumeiona Mbezi Beach tangu inajengeka, tumejenga huko tangu enzi za Nyerere, tumeliona hilo Tangi Bovu tangu lilipokuwepo zima, tumepewa mashamba ya kukatiwa na CCM bure huko siku hizo, Mbezi Beach ilishakongoroka miaka 10 iliyopita.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…