Bara la Afrika kuja na Sarafu yake itakayoitwa Afro au Afric (Afro currency au Afric currency)

Ule mpango wa Putin uliishia wapi?
Achana na putin yule naye yupo kimaslahi... Yule anatumia Africa kuwaumiza wamarekani ni sawa na mwanamke anakuwa na wewe hili kumkomoa Rafiki yake.. kuwa na wewe haimaanishi anakupenda, bali afanikishe jambo lake la kumtambia adui
 
Mbona Euro wameweza na wanauziana na kufanya biashara kwa pesa yao... Hakuna cha tricky hapo, au unamuogopa mmarekani kiasi hicho... Dollar yake ibaki pale pale, ila huku kwetu ndani ya Afrika tufanye biashara kwa pesa yetu
Bado una akili za kitoto ukikua utajua hao ulaya condition za mikopo Yao walikusaini kuilipa Kwa Hela Gani ?


Je world bank atakukopesha akubali umlipe kwa hiyo pesa ?

Halafu Kwa mikopo Ambayo nchi imeshachukua Kila mwezi inalipwa Kwa Dola , Je mtaihudumia vipi ?
 
Confidence hakuna kwa mswahili yaani kila kitu anaona hawezi
Mbona kuiba wwnaweza? Kwanini wasiibe maarifa?
Kweli continent lote linategemea misaada tu kila kukicha
Kuiba wanaweza, ila kuwa na Sarafu yetu wanaona ni jambo ambalo haliwezekaniki [emoji23] Bongo nyosoo
 
Shida sio sarafu bali Wizi, ufisadi na Rushwa
 
Siyo wazo jipya hilo.

"Kwani Ghaddafi alipoleta wazo hilo alisema iitwe vipi?

Unafikiri kilichomuuwa Ghaddafi ni nini?
Hata kipindi cha kudai uhuru watu wengi walikufa lakini haikuzuia watu kuendelea kupigania uhuru... Wewe baki na fikra zako za kuogopa kufanya kisa fulani alifanya akafa... Haya maisha na vitu unavyotumia leo ni sacrifice ya maisha ya watu wengine... Wewe unatakiwa kujua Gadaffi alijikwaa wapi kisha wewe uje na njia mbadala

Sasa wewe baki na Neno Gadaffi alifanya akauwawa... Maisha bila kufanya risk hakuna kitu kipya, aliyegundua moto nae alikufa kwa kuungua lakini hakutuzuia kuendelea kuutumia
 
Time will tell.
Time is the best teacher.
That thing will not work.
Hata Nyerere alipoenda kudai uhuru aliambiwa hawezi kupewa uhuru, lakini leo hii wewe unadunda mtaani bila kuitwa mtumwa... Na unakuja hapa kusema haitawezekana... Hiyo simu yenyewe inayotumia kuna watu waliambiwa hawataweza kutengeneza lakini leo hii wewe ndio unadunda nayo... Sisi tutakukumbusha tu Mwalimu wa Mathe hapa ni wapi
 
Kwa akili zako wewe upo huru hapa bongo ?
 
Shida sio sarafu bali Wizi, ufisadi na Rushwa
Wizi, ufisadi na Rushwa, hivyo sio vitu vya leo... Ni toka enzi ya mababu zetu ambapo hata pesa haikuwepo... Hapa tunaongelea sarafu ya Afrika na si matatizo ya mtu mmoja mmoja
 
Wizi, ufisadi na Rushwa, hivyo sio vitu vya leo... Ni toka enzi ya mababu zetu ambapo hata pesa haikuwepo... Hapa tunaongelea sarafu ya Afrika na si matatizo ya mtu mmoja mmoja
Dogo una miaka mingapi ?
 
Wazo zuri lakini hii itakuwa pigo kubwa sana kwa wamagharibi na mshirika wao U.S , Swali ni je watakubali lifanikiwe tena kwenye bara lenye viongozi wengi mamluki wao na wanalolimudu?
Wenyewe wamevurugwa wanawaza LGBT na uinukaji wa china pia unawachanganya
 
Wizi, ufisadi na Rushwa, hivyo sio vitu vya leo... Ni toka enzi ya mababu zetu ambapo hata pesa haikuwepo... Hapa tunaongelea sarafu ya Afrika na si matatizo ya mtu mmoja mmoja
Acha ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…