Barabara hatarishi huwa na mtelemko mikali au kona nyingi

Upo sahihi kushuka Mtowisa kutoka Sumbawanga kwa kupitia Muze hapo hakuna tena Tanzania nzima! Mtu atakayebisha basi hajawahi kushuka bonde la Rukwa! Gari ikifeli breki inashuka bondeni kama helkopta na kwenda kutua bondeni kama gunia la viazi!
Unaijua vyema wala hujahadithiwa.

Nilikuwa nasali mwanzo mwisho.
 
Asante mkuu kwa nyongeza hiyo
 
Mnaijua ndororo??? nadhani ni hatari zaidi ila hamjaitaja .. mabasi mawili tu yanapanda huo mlima alsaedy na kidinilo.. inapatikana kipande cha ifakara to mahenge ulanga..inakochimbwa rubi,spinal,uno etc.. hutatamani kutazama pembeni na ukikaa nyuma basi unaona mbele limenyanyuka,kona zake ni hatari mno. lushoto hakuna kitu pale burdani inalala na 70 kabisa,kitonga pia 50basi linatembea.. na kwingine ka hizo picha zenu bado hakuna milima hatari..alosoma kwiro secondary atanielewa
 
Asante mkuu kwa nyongeza, ukifanikiwa kupata picha unaweza kutuwekaa hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…