Saad30
JF-Expert Member
- May 26, 2020
- 2,737
- 5,464
Moja kwa moja kwenye mada.
Viongozi wa Mji wa Korogwe hamuoni ile barabara ya kuelekea Hospitali ya Magunga? Barabara mpya ambayo inaonganisha mtaa wa Mountain view na Kanisa la Roma imeanza kuleta shida.
Shimo ambalo limeanza kuonekana litaweza kusababisha ajali usiku na pia uharibifu wa barabara ile maana linazidi kuchimbika na kutanuka pia. Viongozi litazameni hili jambo na pia rekebisheni yale mataa maana usiku ni giza la kutosha barabarani.
Nawapa pongezi kwa utengenezaji wa barabara na kuunganisha pale mlipoishia.
Mungu ibaraki wilaya Korogwe
Mungu ibariki Tanga
Mungu ibariki Tanzania
Mungu mpe afya tele Rais wetu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan.