Barabara inayoelekea kwenye Mahakama Kinondoni,Ofisi za OSHA ina mashimo yanaleta kero, TARURA ipo wapi?

Barabara inayoelekea kwenye Mahakama Kinondoni,Ofisi za OSHA ina mashimo yanaleta kero, TARURA ipo wapi?

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Barabara inayotokea njia Kuu ya Kinondoni(Kawawa road )kuelekea Mahakama ya Kinondoni/Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki, Ofisi za OSHA imearibika na ina mashimo ambayo sio salama jambo ambalo linapeleka madhara ikiwemo kuleta usumbufu kwa wenye magari, ambapo baadhi tumekutana na changamoto ya magari kuaribika kutokana na mawe yaliyopangwa kwenye njia hiyo kwa lengo la kupunguza mashimo.

Changamoto hiyo imedumu kwa muda sasa, watumiaji wengi tunateseka, tulitegemea mpaka sasa mamlaka zingekuwa zimechukua hatua kwa kuboresha maeneo sumbufu.

Kibaya zaidi katikati njia hiyo kuna shimo la chemba ambalo lipo katikati ya barabara limefunuliwa jambo ambalo linaongeza usumbufu kwa watumiaji wa barabara hiyo.

Wito wangu kwa TARURA Kinondoni ni vyema wakafuatilia suala hilo kisha watenge bajeti kwa ajili ya ukarabati kwa haraka, kinyume hivyo kwa hali ilivyo sasa inaonesha mvua zikianza kunyesha kero itakuwa kubwa zaidi.
photo_2025-03-05_08-46-00 (2).jpg

photo_2025-03-05_08-45-59.jpg

photo_2025-03-05_08-46-00.jpg

photo_2025-03-05_08-46-01.jpg

photo_2025-03-10_13-20-49 (2).jpg

photo_2025-03-10_13-22-04.jpg
 
Miaka nenda rudi kipande hiki kiko ovyo

Ova
 
Back
Top Bottom