Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mimi ni Mwananchi wa Manispaa ya Lindi, Mtaa wa Jangwani, kero yangu ni kuwa Barabara inayounganisha Mtaa wa Jangwani na Manispaa (mahala tunapopata huduma zetu za kila siku) imeharibika haifai kwa matumizi ya kiangazi hata masika.
Kibaya zaidi mamlaka inalitambua hili tokea Mwaka 2023, ila wanatupiga danadana nyingi na hakuna kinachofanyika.
Mwaka 2023 aliwahi kuja Mkurugenzi wa Manispaa na Mkuu wa Wilaya lakini hakuna kilichoendelea, barabara ni mbaya haifai kupitika naomba Waziri naye aje ainee.