St. Paka Mweusi
JF-Expert Member
- Sep 3, 2010
- 7,956
- 5,149
Naanza kwa kuwasalimia wakuu. Hapa ntaongelea matukio mawili niliyoyashuhudia kwa macho yangu.. Pia ntaongelea matukio machache niliyoyasikia.
Mwezi mmoja uliopita mida ya saa 11 alfajiri nikiwa napita maeneo ya Mbezi mwisho jirani na stendi ya mabasi ya Magufuli nilishuhudia mwili wa mwanamke ukiwa katikati ya matairi ya nyuma ya Lori( Semi Trailer lenye mzigo) dereva wa Lori hilo akiwa amekimbia na kuacha gari ikiwa imenasa mwili wa mwanamke huyo marehemu.
Siku nne zilizopita tukiwa maeneo ya Kibamba Hospitali muda wa saa nne usiku, Kijana mmoja aliwaaga wenzake kuwa anaenda upande wa pili wa barabara atarudi baada ya muda mfupi.. Alipokuwa akivuka barabara aligongwa na gari ndogo tukishuhudia. Akapoteza maisha palepale.
Miezi miwili iliyopita kijana mmoja ambaye alikuwa katibu wa vijana wa CCM aligongwa akiwa kwenye pikipiki maeneo ya Luguruni na kupoteza maisha palepale.
Miezi kama mitatu iliyopita mama mmoja akiwa anavuka barabara maeneo ya Kibamba CCM aligongwa na Lori(Semi Trailer) na kupoteza maisha palepale.
Sasa nachojiuliza.. TUTASUBIRI MPAKA AFE NANI NDIO TUCHUKUE HATUA..?? Matukio ni mengi sana. Watu wanakufa kwa sababu ya ajali za barabarani. Wahusika wapo wapi? Tukumbuke kuwa barabara hii ni High way inayopita kwenye makazi ya watu. Huyu mwananchi anayetumia barabara hii tunamlinda vipi kama watu wanakufa kwa kugongwa kwenye Zebra Crossings?
USHAURI WANGU KWA TANROADS
Wakandarasi wa TANROADS wabuni vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.
Vivuko hivi vitawasaidia waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, na hata waendesha bodaboda kuvuka barabara hii bila kuathiri madereva wa magari. Na nina imani kuwa tutapunguza vifo vitokanavyo na ajali ka kiasi kikubwa sana.
NAOMBA KUWAKILISHA KWA HESHIMA NA TAADHIMA.