USHAURI WANGU KWA TANROADS
Wakandarasi wa TANROADS wabuni vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.
Pia pembezo kuwepo njia za waenda kwa miguu kama zilivyo ktk barabara za Mandela express way Ubungo mpaka bandarini pia kama ilivyo barabara za Nyerere Road kwenda Airport ya JNIA DSM hata barabara ya Morogoro kuanzia Kisutu, Fire, Magomeni hadi Ubungo zote zipo jijini Dar es Salaam na zimejengwa huku kuna njia za waendao kwa miguu kwa usalama wao na kuondoa vurugu za magari na waendao kwa miguu kuwepo.
Ni jambo la kushangaza barabara zinazojengwa sasa za 'Magufuli' kukosa njia za waendao kwa miguu pande zote mbili kama vile barabara hizo zinapita porini kusipokuwa na makaazi ya watu.
BARABARA YA ZAMANI YENYE USALAMA :
Barabara ya Nyerere Road kutoka Lumumba mpaka Airport ya Julius Nyerere ikiwa na njia za waenda kwa miguu pia service road pembezoni
Barabara ya new bagamoyo jijini Dar es Salaam iliyo na sehemu za wapita miguu pande zote za barabara