Hii mada inakuja kwa mara nyingine humu, tuache siasa tuongee ukweli ili marekebisho yawe ya kisayansi sio kisiasa, Ile ni freeway, pedestrians, bodaboda hawatakiwi kuwepo pale, pia tulete wataalamu watufanyie uchunguzi kama ile barabara imejengwa kwa kuangalia usalama wa watumiaji, kuwekwe pedestrians traffic lights 🚥 ambazo zitatumiwa na binadamu wanaotaka kukatiza ile freeway, kujengwe fixed speed cameras to control speed ya magari, na pia tuweke camera's za kurekodi muda ambao gari ina safiri kutoka point A to B,overspending iwe ni fine kubwa(sio spot fine)ila irekodiwe na kumbukumbu za driver, taa za barabarani pale hazifanyi kazi, tuziweke hizi ili visibility iwe nzuri, tuta zote zile futilia mbali ni usumbufu tu
Na ndicho wanachotaka; kuweka matuta.
Nilifanya utafiti mdogo wa muda wa safari kwa daladala:
Mbezi-Maili Moja= dk 20
Maili Moja-Vigwaza=dk 40
Barabara hii ina tija na ni nzuri sana ila shida ipo kwa Wabongo wanaojiita wazoefu wa mjini kutaka kutumia hii njia kama zamani na watakavyo.
Ni kweli ajali zipo, lakini ni shida ya waenda kwa miguu. Kimsingi, mtu haruhusiwi kuvuka kabla gari haijasimama hata kama ni kwenye zebra.
Dereva anatakiwa apunguze mwendo tu pindi afikapo kwenye zebra na halazimiki kusimama iwapo hajamuona mtu anavuka.
Anayevuka ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha kwamba kwanza ameliona gari na pia dereva amemuona na gari imesimama ndipo avuke.
.................
BARABARA NI ENEO HATARI KABISA, MWENDA KWA MIGUU HUTAKIWI KUCHEZACHEZA AU KUENENDA KIZEMBE KIZEMBE KWENYE ZEBRA AU KANDONI MWA BARABARA.
1. Acha kuvuka barabara ukiwa unaongea na simu
2. Acha kuvuka barabara ukiwa unapiga stori na mwenzako
3. Acha kuvuka barabara ukiwa na headphone masikioni
4. Kwenye kivuko cha waenda kwa miguu simama wima huku ukionesha nia ya kuvuka barabara.
5. Angalia magari barabarani kushoto, kulia na sehemu zote kukuzunguka, na sikiliza. Kwa kufanya hivi dereva atakuona na hivyo kusimama kukuruhusu uvuke.
6. Usitumie eneo la Zebra kama kijiwe cha kupigia stori, kuuza bidhaa, au kuongea na simu.
7. Usitegemee sana uwepo wa Polisi kumwadhibu dereva kwani dereva ataadhibiwa lakini wewe utakuwa umepoteza viungo vyako ukapata ulemavu wa kudumu au ukapata kifo, wakati dereva atalipa 50,000 na kuachiwa.
Zingatia Wajibu wa Mwenda kwa Miguu kwenye Kivuko cha Waenda kwa Miguu Uliowekwa na Sheria
1.
Kif.65(6) kinamtaka mwenda kwa miguu atumie kivuko cha waenda kwa miguu anapotaka kuvuka barabara ikiwa kivuko hicho kipo. Lakini pili, anapovuka avuke kwa umakini (exercise due care);
2.
Kifungu cha 65(7) anapotumia kivuko chenye alama na michoro basi anawajibika kuzingatia yafuatayo:
(a) Kutii maelekezo yaliyotolewa na ishara (mf.taa)
(b) Asisimame katikati ya barabara ikiwa taa zimeruhusu au askari ameruhusu gari zipite.
(c) Asiweke mguu barabarani (shall not step onto the carriage way) kuanza kuvuka bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja.
3.
Kifungu cha 65(8) kinasema mwenda kwa miguu hatakiwi kuenenda barabarani katika namna ambayo ni hatari au inaweza kuwa chanzo cha hatari kwake yeye au kwa mtumiaji mwingine wa barabara.
KUMBUKA kwamba kifungu cha 64A kinamtaka kila mtumiaji wa barabara azingatie umakini na utimamu na wakati wote achukue tahadhari kutohatarisha au kuzuia magari au kuhatarisha watumiaji wengine wa barabara.
DAIMA TAMBUA kuwa barabara ni eneo hatari ambalo chochote kinaweza kutokea:
1. Gari inaweza kuacha njia na kukufuata ulipo hata kama upo nje kabisa ya barabara;
2. Gari inaweza kufeli breki kwenye zebra na bado ukagonjwa na ndio maana sheria inataka kabla hujaanza kuvuka uzingatie umbali na spidi ya gari inayotakiwa kusimama kukupisha
Heshimu barabara, Nenda salama barabarani
RSA Tanzania.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.
..................
Fungo Augustus ▶ RSA TANZANIA(Road Safety Ambassadors)
JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA? Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.
Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.
Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.
Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke
bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja
Kifungu cha 65(10) kinasema
itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.
KWA MINAJILI YA REJEA KIFUNGU CHENYEWE CHA 65(10) Kinasema hivi katika lugha yake asili "(10) Where a pedestrian is using or is about to use a pedestrian crossing, a driver of a vehicle shall stop before a pedestrian crossing on a carriageway which is not regulated by traffic lights, traffic signals or by a police officer."
HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo,
dereva asimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.
Ni matumaini yangu tumeelewana. Mwelimishe na mwenzio.
RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
ZINGATIA: Maelezo haya hayahusishi zile ZEBRA crossings ambazo kabla yake kunakuwa na mchoro chini au alama ya amri iliyoandikwa kabisaaa STOP. Hapa utatakiwa kusimama hata kama hakuna anayevuka.