Barabara ya Kimara mpaka Kibaha itazamwe upya, vifo vya watu kutokana na kugongwa na magari vimekuwa vingi sana

USHAURI WANGU KWA TANROADS
Wakandarasi wa TANROADS wabuni vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.

Pia pembezo kuwepo njia za waenda kwa miguu kama zilivyo ktk barabara za Mandela express way Ubungo mpaka bandarini pia kama ilivyo barabara za Nyerere Road kwenda Airport ya JNIA DSM hata barabara ya Morogoro kuanzia Kisutu, Fire, Magomeni hadi Ubungo zote zipo jijini Dar es Salaam na zimejengwa huku kuna njia za waendao kwa miguu kwa usalama wao na kuondoa vurugu za magari na waendao kwa miguu kuwepo.


Ni jambo la kushangaza barabara zinazojengwa sasa za 'Magufuli' kukosa njia za waendao kwa miguu pande zote mbili kama vile barabara hizo zinapita porini kusipokuwa na makaazi ya watu.

BARABARA YA ZAMANI YENYE USALAMA :
Barabara ya Nyerere Road kutoka Lumumba mpaka Airport ya Julius Nyerere ikiwa na njia za waenda kwa miguu pia service road pembezoni


Barabara ya new bagamoyo jijini Dar es Salaam iliyo na sehemu za wapita miguu pande zote za barabara

 
Wangechimba chini mvua ikinyesha mpite wapi? Ungezingatia miundombinu ya maji taka hapa Dar usingeongea kupinga wajenzi na idea ile. Ukitaka ukwepe hayo tiyari unaingia gharama vilevile. Ukijenga kupitia chini maintenance inakuwa kubwa naamini hivyo
 
Hapo ndio utaonekana umuhimu wa kuwepo njia mbadala yenye Road toll, ambayo huko nyuma NSSF kupitia Dau walipeleka mapendekezo serilikali ikakataa, High way huwa kuna speed zake na ni hatari sana wakati mwingine hata anaendesha mwendo wa Pole Pole anakuwa hatarini
 
Kivuko kikubwa cha watu kipo pale Mbezi mwisho, kwanini wasipite kwenye kivuko? Sio kila kitu kulaumu serikali, watu wengine wabishi sana..

Na dunia nzima, hakuna High way yenye matuta, hiyi itakuwa kifo kwa watu na magari mengi mno, haiwezekani kabisa kabisa highway kuweka tuta, utaua watu kwa ajali kila siku, sbb gari zitaua balaa, high haiwezekani kuweka matuta na haipo kokote kule, that is most dangerous.

Watu waache kiburi na ubishi, watumie kivuko cha miguu kikubwa na kizuri kipo pale.
 

Zebra cross kwenye highway ni mambo ya zamani na sio solution sahihi. Vivuko vya juu ya chini ya barabara ndio solution sahihi. Tatizo vibaka nao wanapenda hivi vivuko kama manzese darajani enzi hizo.
 
Hiyo ni highway lazima watu wawe makini. Usipokua makini hata barabara za ndani tu utagongwa na kufa
 
Walikuja wazungu wanaojenga barabara za Qatar zitakazohudumia world cup! wakasema hiyo barabara inamiss vitu vingi muhimu.
 
Mkuu hata mimi nashanga !!! Serikali imejenga daraja kwa waenda kwa miguu lakini hao watu halitumii na wang'ang"ana kuvuka barabarani kupishana na magari.
 
Zebra cross kwenye highway ni mambo ya zamani na sio solution sahihi. Vivuko vya juu ya chini ya barabara ndio solution sahihi. Tatizo vibaka nao wanapenda hivi vivuko kama manzese darajani enzi hizo.
Vibaka sioni kuwa ni tatizo kama tutakabidhi vivuko hivyo kwa serikali ya mtaa husika.. Ni suala la kuwatumia vijana wa ulinzi shirikishi wa eneo husika wenye nidhamu wahakikishe usalama wa vivuko hivyo..
 
Mkuu hata mimi nashanga !!! Serikali imejenga daraja kwa waenda kwa miguu lakini hao watu halitumii na wang'ang"ana kuvuka barabarani kupishana na magari.
Upo sawa katika maeneo yenye vivuko.. Lakini kuna maeneo mengi yasiyo na vivuko.. Tunawasaidiaje watembea kwa miguu na madereva katika maeneo hayo..??
 
Wafe tu, wajinga ni wengi sana nchi hii
 
Wapige tu fensi kublock njia kama buguruni au pale ubungo mataa
 
Zebra crossing Kwa nchi yetu hatujawah kuheshimiwa..
 
Miundombinu ya Dar es Salaam haifai kuchimba chini kujenga vivuko vya barabara hususani kipindi cha mvua.
 
Kuna mtu aligongwa pale mbezi mwisho junction ya Goba. truck lilimsaga na nyama nyama zimetapakaa..wakati napita alfajili saa kumi na moja .yaani siku yangu nzima ilivurugika kuona kifo kile.. hiyo barabara ni hatari Sana ..vifo ni vingi Sana hicho kipande

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…