Dah- kuna jamaa aligongwa hapo akadondoka bila kujua mguu umekatika, ile kunyanyuka tu akadondoka chini.Mm bunfsi nilinusurika kugongwa na alphad stop over
... safi sana! Haya ndio mambo wananchi wanatakiwa waelimishwe daily kwenye media na hata mabango makubwa barabarani kila penye kivuko - kazi ya TANROADS hiyo ila hawafanyi.RSA Tanzania
BARABARA NI ENEO HATARI KABISA, MWENDA KWA MIGUU HUTAKIWI KUCHEZACHEZA AU KUENENDA KIZEMBE KIZEMBE KWENYE ZEBRA AU KANDONI MWA BARABARA.
1. Acha kuvuka barabara ukiwa unaongea na simu
2. Acha kuvuka barabara ukiwa unapiga stori na mwenzako
3. Acha kuvuka barabara ukiwa na headphone masikioni
4. Kwenye kivuko cha waenda kwa miguu simama wima huku ukionesha nia ya kuvuka barabara.
5. Angalia magari barabarani kushoto, kulia na sehemu zote kukuzunguka, na sikiliza. Kwa kufanya hivi dereva atakuona na hivyo kusimama kukuruhusu uvuke.
6. Usitumie eneo la Zebra kama kijiwe cha kupigia stori, kuuza bidhaa, au kuongea na simu.
7. Usitegemee sana uwepo wa Polisi kumwadhibu dereva kwani dereva ataadhibiwa lakini wewe utakuwa umepoteza viungo vyako ukapata ulemavu wa kudumu au ukapata kifo, wakati dereva atalipa 50,000 na kuachiwa.
Zingatia Wajibu wa Mwenda kwa Miguu kwenye Kivuko cha Waenda kwa Miguu Uliowekwa na Sheria
1. Kif.65(6) kinamtaka mwenda kwa miguu atumie kivuko cha waenda kwa miguu anapotaka kuvuka barabara ikiwa kivuko hicho kipo. Lakini pili, anapovuka avuke kwa umakini (exercise due care);
2. Kifungu cha 65(7) anapotumia kivuko chenye alama na michoro basi anawajibika kuzingatia yafuatayo:
(a) Kutii maelekezo yaliyotolewa na ishara (mf.taa)
(b) Asisimame katikati ya barabara ikiwa taa zimeruhusu au askari ameruhusu gari zipite.
(c) Asiweke mguu barabarani (shall not step onto the carriage way) kuanza kuvuka bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja.
3. Kifungu cha 65(8) kinasema mwenda kwa miguu hatakiwi kuenenda barabarani katika namna ambayo ni hatari au inaweza kuwa chanzo cha hatari kwake yeye au kwa mtumiaji mwingine wa barabara.
KUMBUKA kwamba kifungu cha 64A kinamtaka kila mtumiaji wa barabara azingatie umakini na utimamu na wakati wote achukue tahadhari kutohatarisha au kuzuia magari au kuhatarisha watumiaji wengine wa barabara.
DAIMA TAMBUA kuwa barabara ni eneo hatari ambalo chochote kinaweza kutokea:
1. Gari inaweza kuacha njia na kukufuata ulipo hata kama upo nje kabisa ya barabara;
2. Gari inaweza kufeli breki kwenye zebra na bado ukagonjwa na ndio maana sheria inataka kabla hujaanza kuvuka uzingatie umbali na spidi ya gari inayotakiwa kusimama kukupisha
Heshimu barabara, Nenda salama barabarani
RSA Tanzania.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.
Mkuu hapo kwenye gari kusimama kwenye Zebra napingana na wewe.. Dereva unatakiwa usimame kwenye Zebra crossing hata kama hakuna mtu anayevuka.. Kuna mama mmoja Veko mkoani Iringa mwaka 2018 alikuja kusisitiza sheria hiyo.. Madereva wengi Walikamatwa.. Binafsi kuna siku nipo na Brevis imeiva speed 140 maeneo ya Kiluvya kwa Komba jamaa wakanipiga mkono.. Nikamuachia buku 2 nikatembea.. Na alikuwa amesimamisha magari mengi tu kwa kosa hilo la kutosimama kwenye Zebra crossing..Na ndicho wanachotaka; kuweka matuta.
Nilifanya utafiti mdogo wa muda wa safari kwa daladala:
Mbezi-Maili Moja= dk 20
Maili Moja-Vigwaza=dk 40
Barabara hii ina tija na ni nzuri sana ila shida ipo kwa Wabongo wanaojiita wazoefu wa mjini kutaka kutumia hii njia kama zamani na watakavyo.
Ni kweli ajali zipo, lakini ni shida ya waenda kwa miguu. Kimsingi, mtu haruhusiwi kuvuka kabla gari haijasimama hata kama ni kwenye zebra.
Dereva anatakiwa apunguze mwendo tu pindi afikapo kwenye zebra na halazimiki kusimama iwapo hajamuona mtu anavuka.
Anayevuka ndiye mwenye jukumu la kuhakikisha kwamba kwanza ameliona gari na pia dereva amemuona na gari imesimama ndipo avuke.
.................
BARABARA NI ENEO HATARI KABISA, MWENDA KWA MIGUU HUTAKIWI KUCHEZACHEZA AU KUENENDA KIZEMBE KIZEMBE KWENYE ZEBRA AU KANDONI MWA BARABARA.
1. Acha kuvuka barabara ukiwa unaongea na simu
2. Acha kuvuka barabara ukiwa unapiga stori na mwenzako
3. Acha kuvuka barabara ukiwa na headphone masikioni
4. Kwenye kivuko cha waenda kwa miguu simama wima huku ukionesha nia ya kuvuka barabara.
5. Angalia magari barabarani kushoto, kulia na sehemu zote kukuzunguka, na sikiliza. Kwa kufanya hivi dereva atakuona na hivyo kusimama kukuruhusu uvuke.
6. Usitumie eneo la Zebra kama kijiwe cha kupigia stori, kuuza bidhaa, au kuongea na simu.
7. Usitegemee sana uwepo wa Polisi kumwadhibu dereva kwani dereva ataadhibiwa lakini wewe utakuwa umepoteza viungo vyako ukapata ulemavu wa kudumu au ukapata kifo, wakati dereva atalipa 50,000 na kuachiwa.
Zingatia Wajibu wa Mwenda kwa Miguu kwenye Kivuko cha Waenda kwa Miguu Uliowekwa na Sheria
1. Kif.65(6) kinamtaka mwenda kwa miguu atumie kivuko cha waenda kwa miguu anapotaka kuvuka barabara ikiwa kivuko hicho kipo. Lakini pili, anapovuka avuke kwa umakini (exercise due care);
2. Kifungu cha 65(7) anapotumia kivuko chenye alama na michoro basi anawajibika kuzingatia yafuatayo:
(a) Kutii maelekezo yaliyotolewa na ishara (mf.taa)
(b) Asisimame katikati ya barabara ikiwa taa zimeruhusu au askari ameruhusu gari zipite.
(c) Asiweke mguu barabarani (shall not step onto the carriage way) kuanza kuvuka bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja.
3. Kifungu cha 65(8) kinasema mwenda kwa miguu hatakiwi kuenenda barabarani katika namna ambayo ni hatari au inaweza kuwa chanzo cha hatari kwake yeye au kwa mtumiaji mwingine wa barabara.
KUMBUKA kwamba kifungu cha 64A kinamtaka kila mtumiaji wa barabara azingatie umakini na utimamu na wakati wote achukue tahadhari kutohatarisha au kuzuia magari au kuhatarisha watumiaji wengine wa barabara.
DAIMA TAMBUA kuwa barabara ni eneo hatari ambalo chochote kinaweza kutokea:
1. Gari inaweza kuacha njia na kukufuata ulipo hata kama upo nje kabisa ya barabara;
2. Gari inaweza kufeli breki kwenye zebra na bado ukagonjwa na ndio maana sheria inataka kabla hujaanza kuvuka uzingatie umbali na spidi ya gari inayotakiwa kusimama kukupisha
Heshimu barabara, Nenda salama barabarani
RSA Tanzania.
Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.
..................
Fungo Augustus ▶ RSA TANZANIA(Road Safety Ambassadors)
JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA? Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.
Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.
Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.
Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja
Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.
KWA MINAJILI YA REJEA KIFUNGU CHENYEWE CHA 65(10) Kinasema hivi katika lugha yake asili "(10) Where a pedestrian is using or is about to use a pedestrian crossing, a driver of a vehicle shall stop before a pedestrian crossing on a carriageway which is not regulated by traffic lights, traffic signals or by a police officer."
HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo, dereva asimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.
Ni matumaini yangu tumeelewana. Mwelimishe na mwenzio.
RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
ZINGATIA: Maelezo haya hayahusishi zile ZEBRA crossings ambazo kabla yake kunakuwa na mchoro chini au alama ya amri iliyoandikwa kabisaaa STOP. Hapa utatakiwa kusimama hata kama hakuna anayevuka.
Sidhani kama unapingana na mimi, isipokuwa unapingana na sheriaMkuu hapo kwenye gari kusimama kwenye Zebra napingana na wewe.. Dereva unatakiwa usimame kwenye Zebra crossing hata kama hakuna mtu anayevuka.. Kuna mama mmoja Veko mkoani Iringa mwaka 2018 alikuja kusisitiza sheria hiyo.. Madereva wengi Walikamatwa.. Binafsi kuna siku nipo na Brevis imeiva speed 140 maeneo ya Kiluvya kwa Komba jamaa wakanipiga mkono.. Nikamuachia buku 2 nikatembea.. Na alikuwa amesimamisha magari mengi tu kwa kosa hilo la kutosimama kwenye Zebra crossing..
... na hicho ndicho kinachotakiwa na sio kuweka mazebra kila baada ya 25m! Imagine vituo vya mwendokasi; ilitegemewa wasafiri wangekuwa wanaingia na kutoka vituoni through tunnels lakini ujinga uliofanyika ndio kama hivyo ni foleni za magari mwanzo mwisho! Mji umejaa foleni all the way!
Huo ushauri ni murua sana lakini haumo kwenye notisi walizofundishiwa wataalam wetu wa mabarabara. Nashauri uuanzishie uzi wake ili usome kirahisi.Naanza kwa kuwasalimia wakuu. Hapa ntaongelea matukio mawili niliyoyashuhudia kwa macho yangu.. Pia ntaongelea matukio machache niliyoyasikia.
Mwezi mmoja uliopita mida ya saa 11 alfajiri nikiwa napita maeneo ya Mbezi mwisho jirani na stendi ya mabasi ya Magufuli nilishuhudia mwili wa mwanamke ukiwa katikati ya matairi ya nyuma ya Lori( Semi Trailer lenye mzigo) dereva wa Lori hilo akiwa amekimbia na kuacha gari ikiwa imenasa mwili wa mwanamke huyo marehemu.
Siku nne zilizopita tukiwa maeneo ya Kibamba Hospitali muda wa saa nne usiku, Kijana mmoja aliwaaga wenzake kuwa anaenda upande wa pili wa barabara atarudi baada ya muda mfupi.. Alipokuwa akivuka barabara aligongwa na gari ndogo tukishuhudia. Akapoteza maisha palepale.
Miezi miwili iliyopita kijana mmoja ambaye alikuwa katibu wa vijana wa CCM aligongwa akiwa kwenye pikipiki maeneo ya Luguruni na kupoteza maisha palepale.
Miezi kama mitatu iliyopita mama mmoja akiwa anavuka barabara maeneo ya Kibamba CCM aligongwa na Lori(Semi Trailer) na kupoteza maisha palepale.
Sasa nachojiuliza.. TUTASUBIRI MPAKA AFE NANI NDIO TUCHUKUE HATUA..?? Matukio ni mengi sana. Watu wanakufa kwa sababu ya ajali za barabarani. Wahusika wapo wapi? Tukumbuke kuwa barabara hii ni High way inayopita kwenye makazi ya watu. Huyu mwananchi anayetumia barabara hii tunamlinda vipi kama watu wanakufa kwa kugongwa kwenye Zebra Crossings?
USHAURI WANGU KWA TANROADS
Wakandarasi wa TANROADS wabuni vivuko vya kupita chini ya barabara ambavyo ni nafuu kuvijenga ikilinganishwa na madaraja ya kupita juu ambayo yana gharama kubwa zaidi.
Vivuko hivi vitawasaidia waenda kwa miguu, waendesha baiskeli, na hata waendesha bodaboda kuvuka barabara hii bila kuathiri madereva wa magari. Na nina imani kuwa tutapunguza vifo vitokanavyo na ajali ka kiasi kikubwa sana.
NAOMBA KUWAKILISHA KWA HESHIMA NA TAADHIMA.
... what if mwenda kwa miguu akagongwa pasipo na alama au kivuko cha waenda kwa miguu? Sheria inasemaje Mkuu?Sidhani kama unapingana na mimi, isipokuwa unapingana na sheria
Fungo Augustus ▶ RSA TANZANIA(Road Safety Ambassadors)
JE NI WAKATI GANI NISIMAME KWENYE ZEBRA CROSSINGS AU JE NI AMRI KUSIMAMA KWENYE ZEBRA HATA KAMA HAKUNA MWENDA KWA MIGUU ANAYEVUKA? Sheria inasemaje?
Sheria ya usalama barabarani kifungu cha 65 kinahusu vivuko vya waenda kwa miguu, yaani pedestrian crossings.
Kifungu cha 65(1) kinamtaka mhandisi mkuu kusimika alama za vivuko vya waenda kwa miguu mahali panapofaa barabarani.
Kifungu cha 65(2) kinatamka kwamba mahali popote ambapo alama itakuwa imewekwa itachukuliwa kuwa imewekwa kihalali na itakuwa halali isipokuwa kama itakanushwa au kuthibitishwa vinginevyo.
Kifungu cha 65(6) kinamtaka kila anayetumia kivuko cha waenda kwa miguu kufanya hivyo kwa tahadhari kubwa na atumia kivuko hicho kuvuka barabara. Aidha kifungu cha 65(7) kinamtaka mtumiaji kivuko huyo kutokanyaga barabara ili avuke bila kuzingatia umbali na spidi ya magari yanayokuja
Kifungu cha 65(10) kinasema itakapotokea mtembea kwa miguu anatumia au anataka kutumia kivuko cha waenda kwa miguu, dereva wa gari atasimama kabla ya kivuko hicho ambacho hakiongozwi na taa za barabarani, ishara za barabarani au askari. [Hivi vivuko vinavyokuwa vimechorwa barabarani kwa mistari ya pundamilia ambapo mtu anavuka bila usimamizi wa askari au maelekezo ya taa]. Dereva ataendelea tu na safari ikiwa atajiridhisha kuwa hakuna mtembea kwa miguu anayetumia(anayevuka) au anakusudia kuvuka barabara.
KWA MINAJILI YA REJEA KIFUNGU CHENYEWE CHA 65(10) Kinasema hivi katika lugha yake asili "(10) Where a pedestrian is using or is about to use a pedestrian crossing, a driver of a vehicle shall stop before a pedestrian crossing on a carriageway which is not regulated by traffic lights, traffic signals or by a police officer."
HIVYO BASI, JIBU NI KWAMBA sio lazima dereva asimama kwenye kila zebra crossings hata kama hakuna anayevuka, dereva atapunguza mwendo na kuangalia iwapo kuna mtu anavuka au ananuia kuvuka, kama hakuna ataendelea na safari. Kwa hiyo, dereva asimama kwenye eneo kabla ya zebra crossing pale wakati wote ambapo kuna mtu au watu wanavuka au wanakusudia kuvuka.
Ni matumaini yangu tumeelewana. Mwelimishe na mwenzio.
RSAadmin1
RSA TANZANIA
USALAMA BARABARANI NI JUKUMU LETU SOTE.
ZINGATIA: Maelezo haya hayahusishi zile ZEBRA crossings ambazo kabla yake kunakuwa na mchoro chini au alama ya amri iliyoandikwa kabisaaa STOP. Hapa utatakiwa kusimama hata kama hakuna anayevuka.
... what if mwenda kwa miguu akagongwa pasipo na alama au kivuko cha waenda kwa miguu? Sheria inasemaje Mkuu?
Ukisoma kifungu cha 65 cha Sheria ya usalama Barabarani, kwa ujumla kinamtaka mwenda kwa miguu kuwa makini barabarani na asitembee au kufanya vitendo ambavyo vitahatarisha afya yake na au watumiaji wengine wa barabara.... what if mwenda kwa miguu akagongwa pasipo na alama au kivuko cha waenda kwa miguu? Sheria inasemaje Mkuu?
Kwahiyo huyo mama, ndiye aliendika sheria za usalama barabarani, kivuko kiko sehemu ya wazi, unaona hakuna mtu, anehitaji kuvuka, usimame ili iweje.Mkuu hapo kwenye gari kusimama kwenye Zebra napingana na wewe.. Dereva unatakiwa usimame kwenye Zebra crossing hata kama hakuna mtu anayevuka.. Kuna mama mmoja Veko mkoani Iringa mwaka 2018 alikuja kusisitiza sheria hiyo.. Madereva wengi Walikamatwa.. Binafsi kuna siku nipo na Brevis imeiva speed 140 maeneo ya Kiluvya kwa Komba jamaa wakanipiga mkono.. Nikamuachia buku 2 nikatembea.. Na alikuwa amesimamisha magari mengi tu kwa kosa hilo la kutosimama kwenye Zebra crossing..
Alisimamia hilo na madereva walitii..Kwahiyo huyo mama, ndiye aliendika sheria za usalama barabarani, kivuko kiko sehemu ya wazi, unaona hakuna mtu, anehitaji kuvuka, usimame ili iweje.
Tatizo madereva hatufahamu, baadhi ya vibao barabarani, mita hamsini kabla ya zebra, huwekwa kibao, kinachomtahadharisha dereva, mbele kuna kibao, cha waenda kwa miguu siyo amri, sasa ulazima wa kusimama hata kama zebra haina mvukaji inatoka wapi.
Great explanation! Mkuu wewe ni mzamivu wa sheria za barabarani. Kama wote dereva na mwenda kwa miguu wako responsible mbele ya sheria haijakaa sawasawa faini wanapigwa madereva peke yao!Ukisoma kifungu cha 65 cha Sheria ya usalama Barabarani, kwa ujumla kinamtaka mwenda kwa miguu kuwa makini barabarani na asitembee au kufanya vitendo ambavyo vitahatarisha afya yake na au watumiaji wengine wa barabara.
Na mwenda kwa miguu hatakiwi hata kuweka mguu wake barabarani iwapo anaona gari zina mwendo mkali na pia ahakikishe gari zimesimama then avuke.
Dereva anaambiwa apunguze mwendo kwenye vivuko na asimame iwapo kuna watu wanavuka au wanataka kuvuka. Iwapo hakuna, dereva anaruhusiwa kuendelea na safari.
Sasa je, mtu akigongwa kwenye eneo lisilo na zebra inakuwaje?
Dereva anaweza akabanwa kwenye mwendo, kwamba pengine mwendo wake ulikuwa mkali kuliko ilivyotakiwa. Lakini, pia iwapo kosa ni mwendo kasi, itafuatiwa na kosa la kuendesha gari bila kujali watumiaji wengine wa barabara, likifuatiwa na kosa la kusababisha majeraha (ama kifo), na pia kosa la kuharibu mali (gari).
Mara nyingi makosa ya barabarani ni fine zisizozidi laki 3.
Na pia ukiisoma Sheria ya Usalama Barabarani, inamtetea sana dereva, na inampa mtembea kwa miguu jukumu kubwa zaidi la kuhakikisha usalama wake.
Kwa hiyo, kimsingi, derava akishagonga jukumu la kwanza ni yeye kwenda kituoni kuripoti ajali. Na hapa ndipo dereva huwekwa lockup kwa usalama wake na polisi kushughulika na ajali husika.
Cha msingi, raia wawe makini barabarani kwa sababu wao ndiyo wenye jukumu kubwa zaidi na sheria haipo upande wao sana.
Haki ya aliyeumia kwa kugongwa ikoje?
Majeruhi anatakiwa afungue kesi ya madai mahakamani kudai fidia, na ataambatanisha riport ya polisi na au hukumu ya mahakama yenye kuonyesha kosa la dereva na tukio la ajali.
Elimu kwa wote; drivers na wasio drivers. Hapo ndipo tunapokosea kudhani drivers ndio wavunja sheria peke yao.Mada hii itakuwa mada mtambuka law maana kwamba hii barabara ni highway roads na ina ubora wa kimataifa so TANROADS watoe Elimu kwa drivers pamoja na kuja na wazo jipya
Mfano mwendazake alitaka mpaka service roads kulia na kushoto zitengenezwe hizo ndio zingetumika kwa ajili ya boda boda baiskel na watembea kwa miguu
Pia kuwe na culvert pit roads special kwa wavuka kwa miguu kutoka kushoto kwenda kulia
Hapo tatizo lingekwisha kabisaa na tungewatoa madereva wa malori kwenye lawama zisizo na msingi kila uchao
Hao walioweza wameweza kutokana na kumudu gharama na uweledi, sisi je?Labda sababu ya gharama lakini sio kwamba haifai. Watu wamechimba chini ya mito mikubwa na bahari ndio ishindikane Dar? Sio kweli.