Barabara ya Mabwepande jinsi ilivyotengwa na CCM

Kwani wananchi walikua wapi wakati wanaporwa haki yao ya msingi, walichukua hatua gani zaidi ya kumsifia huyu mwendazake.
Mkuu Hawa watu wanaodhulumiwa haki zao huwa wanaisaka Sana haki zao...ila huwa wanaginga mwamba kwa wahusika kwani hawawasaidii chochote
 
Ukiwauliza juu ya maswali haya hawawezi kukujibu wanabaki kusema tuwe wavimilivu mpaka lini?
Wameitenga sana
Wananchi wameridhika

Ila wasije na ngonjera hii ya barabara kwa ajili ya kupata kura
 
Mwanzoni walisema nileteeni Gwajima....
 
Kibamba ni jina la jimbo lenyewe,kiluvya pia ipo jimbo la kibamba,hilo jimbo la kibamba hasa kata ya kwembe mbunge na diwani wake toka walipochaguliwa hamna walichofanya na hata kuonekana maeneo hayo,kata ya kwembe kuna uwezekano ndio kata duni zaidi ndani ya dar
 
Sitoshangaa muda ukifika wakianza ngonjera kuwaalaghai tena wananchi maskini
 
Ni AsKofu WA Kanisa muda mwingi yupo na Masala ya Kondoo zake. Akizuka Kawe anazukia Waendesha Bajaj na Bodaboda akitumaini hili ninkundi Kubwa la kujipatia Kura ukiwawezesha Maokoto kidogo.
Mwaka huu wote hao wamestuka

Wajipange upya
 

Mkuu kwa maoni yangu naona uwekwe utaratibu wa lazima kuwa katika jumla ya urefu wa kilomita za barabara zote ambazo Tanroad wanasimamia nchini kwa mwaka kuwepo asilimia 30% ambayo itaenda kujenga Barabara za majiji yetu ambayo ni Ilala(Dar es salaam) , Dodoma, Mwanza, Mbeya, Tanga na Arusha.

Hebu fikiria kwa pato ambalo Jijini la Ilala (Dar es salaam) inaliingizia taifa letu ingekuwa kwa mwaka inapata kilomita 250 tu ambazo kilomita 50 zikagawanywa kwa kila Wilaya. Fikiria ni jinsi gani jiji la Ilala(Dar es salaam) lingebadilika!

Barabara za jiji la Ilala (Dar es salaam) ndani ya wilaya moja zimezidi sana ni kilomita 7 au 8 kwa barabara moja, katika kilomita 50 ingeweza kumaliza sehemu kubwa. Kwa awamu mmoja tatizo la barabara litakuwa limeisha.

Majiji mengine yakipata kilomita 50, kwa awamu moja nayo yatakuwa yamemaliza tatizo la barabara kabisa.

Vinginevyo tutakesha na madimbwi, Mashimo miaka nenda rudi kitu ambacho ni hasara kubwa kwa Taifa.

Nawasilisha. Ijumaa Kareem!
 
Huko mbunge siyo Rashid kweli? Anawapeleka wananchi ziarani Japan huku hawana barabara
 
Watu washachoka mm tangu kitambo nilivyoondoka mpk Leo.....
Ni kuwa na subira tu

Itajengwa kuanzia Mbezi kupitia Mpigi Magoe, Mabwepande mpaka Bunju

Pale Mpigi Chama kutajengwa kipande kitakachoenda mpaka Kibamba na daraja lilishajengwa

Lengo la serikali kwa sasa ni kutaka kuwasaidia wananchi wa Dar na viunga vyake kuwa na urahisi wa kufika Magufuli Bus Terminal na hospitali ya Mloganzila

Kwa hiyo barabara ya Mabwepande ni miongoni mwa barabara itakayojengwa kutimiza lengo hilo

Inasubiriwa mradi wa maji ukamilike kwanza ambao tayari umeshafika Mpigi
 
Ushauri Bora kabisa sijui Kam Mzee wa kuchunga kondoo kama atalifikisha hili

Hii barabara ingekuwa ipo kwenye mkakati ingejengwa 2019 ila Kila siku wananchi wanaandaliwa nyimbo za mapambio Tu
 
Huko mbunge siyo Rashid kweli? Anawapeleka wananchi ziarani Japan huku hawana barabara
Huku ni mchunga mbuzi Yule wa kawe...kazi ukutembelea bodaboda na kuwabless buku 5 za mafuta ila kuhusu barabara Hana muda nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…