Kuna makampuni ya kichina yakipewa kandarasi ya kujenga barabara ujenzi wake unakuwa tofauti na wachina wengine. Barabara za makampuni mengine zinabomoka haraka na makampuni mengine hazibomoki haraka walau miaka kumi zinadumu ila wengine miaka kumi haifiki barabara hutatapakaa viraka vitupu na zingine hata kuweka viraka haiwezekani. Linganisha makampuni ya kichina ya SIETCO na CHICO, haya makampuni yanatofautiana sana kujenga barabara. Ipo kampuni nyingine ya CGC, hizi kampuni za kichina hujenga barabara kwa bajeti wanazozijua wao kwa kilometa walizopewa kujenga. Hapa utakuta kilometa alizojenga mmoja wao barabara inakuwa imara kwa miaka mingi na mwingine kilometa alizojenga hazidumu muda mrefu, lami inamemenyuka na kuwa mashimo. Ujenzi hutofautiana kampuni na kampuni. Mwingine akipewa tenda anafukua na kuondoa udongo wa juu na kuweka mwingine kwa matabaka huku mwingine yeye hushindilia udongo alioukuta na kuongeza tabaka moja juujuu kisha lami, huyu ndiye barabara anazojenga hubomoka baada ya miaka michache