Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Saa kumi na nusu ndo tunaikuta foleni ya Kongowe, imeanzia nyuma ya shule ya St Matthews. Hiyo foleni imechukua dk kama 45 hadi kufika makutano ya Kongowe kwenda Kigamboni.
Kwenda Kigamboni hakupitiki maana kuna daladala kama saba zimesimama hadi katikati mwa barabara, zinapakia na kushusha abiria.
Na toka Kigamboni kuna trela inashindwa kuingia barabara kuu, maana imezongwa na bajaji na gari ndogo zinazo jichomeka.
Pale kwenye kadaraja magari zaidi ya 20 kila moja inajaribu kuingiza pua ili ipite.
Hapo foleni ya saa moja na nusu nzimaa na kagiza kanaanza kuingia, na ni saa moja kasoro.
Tumefika Mbagala ndo tunakuta ile barabara ya 2 lanes kwenda mjini, sasa ni half lane. Lane moja nzima ni machinga, nusu lane ni daladala zinazopakia abiria.
Hapo ni kilometa nzima na zaidi. Na foleni hapo ni nusu saa na natazama saa yangu ni saa moja na nusu, tayari ni masaa matatu toka Kongowe.
Hadi kushuka basi kuingia gari dogo Mwenge nafika saa tatu!
Nikifikiria, safari toka Lindi hadi Kongowe masaa manne na nusu, lakini toka Kongowe hadi mjini ni masaa matatu au manne.
Halafu tunasema tunainua mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara, we are joking!
Kwa ufupi, Barabara za kutoka Mbagala - Kongowe kwakweli ipo katika hali mbaya, barabara ni finyu (njia moja) na imejaa mashimo jambo ambalo linapelekea uwepo wa foleni.
Ikizingatiwa njia hiyo ni njia kuu ambayo inaunganisha Mkoa wa Dar na Mikoa mingine ya Kusini, lakini pia ni njia inayotegemewa kupitisha malighafi na bidhaa za viwanda kutoka kwenye viwanda vilivyopo ukanda wa Pwani hususani Wilaya ya Mkuranga.