KERO Barabara ya Mbagala hadi Kongowe ni nyembamba, ina mashimo na inasababisha foleni mara nyingi

KERO Barabara ya Mbagala hadi Kongowe ni nyembamba, ina mashimo na inasababisha foleni mara nyingi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Nimetoka Lindi leo kabla tu ya mchana na basi letu limeenda mwendo mzuri tu! Hata Vikindu foleni haikuwepo.

Saa kumi na nusu ndo tunaikuta foleni ya Kongowe, imeanzia nyuma ya shule ya St Matthews. Hiyo foleni imechukua dk kama 45 hadi kufika makutano ya Kongowe kwenda Kigamboni.

Kwenda Kigamboni hakupitiki maana kuna daladala kama saba zimesimama hadi katikati mwa barabara, zinapakia na kushusha abiria.

Na toka Kigamboni kuna trela inashindwa kuingia barabara kuu, maana imezongwa na bajaji na gari ndogo zinazo jichomeka.
Sie haoo tukaenda barabara ya Mbagala na huko ndo tukakuta foleni ya kufa mtu! Kale kadaraja kabla ya kupanda kilima cha kuingia Mbagala kamezongwa.

Pale kwenye kadaraja magari zaidi ya 20 kila moja inajaribu kuingiza pua ili ipite.

Hapo foleni ya saa moja na nusu nzimaa na kagiza kanaanza kuingia, na ni saa moja kasoro.

Tumefika Mbagala ndo tunakuta ile barabara ya 2 lanes kwenda mjini, sasa ni half lane. Lane moja nzima ni machinga, nusu lane ni daladala zinazopakia abiria.

Hapo ni kilometa nzima na zaidi. Na foleni hapo ni nusu saa na natazama saa yangu ni saa moja na nusu, tayari ni masaa matatu toka Kongowe.

Hadi kushuka basi kuingia gari dogo Mwenge nafika saa tatu!

Nikifikiria, safari toka Lindi hadi Kongowe masaa manne na nusu, lakini toka Kongowe hadi mjini ni masaa matatu au manne.

Halafu tunasema tunainua mikoa ya kusini, Lindi na Mtwara, we are joking!

Kwa ufupi, Barabara za kutoka Mbagala - Kongowe kwakweli ipo katika hali mbaya, barabara ni finyu (njia moja) na imejaa mashimo jambo ambalo linapelekea uwepo wa foleni.

Ikizingatiwa njia hiyo ni njia kuu ambayo inaunganisha Mkoa wa Dar na Mikoa mingine ya Kusini, lakini pia ni njia inayotegemewa kupitisha malighafi na bidhaa za viwanda kutoka kwenye viwanda vilivyopo ukanda wa Pwani hususani Wilaya ya Mkuranga.
Hayupo atakae kusikiliza my be miaka 20 ijayo....

Unajua barabara hiyo baadae itakua crusual Sana hata Sasa Ila haitabiriki..
 
Mhindi ananipa nauli ya laki na thelathini kwena kazini na kurudi nyimbani mwanambaya mkuranga yote inaisha kutoka na foleni za kipuuzi wakati mwingine inanilazimu kupanda pikipiki kutoka nyumbani hadi kazini maeneo ya sokoka
 
Hahaha kazi za wakandarasi wa ndani hizo. Waliishalipana wana kula raha tu huko waliko.
 
Back
Top Bottom