KERO Barabara ya Mbalizi – Iwiji (Mbeya Vijijini) ni kero kubwa, haina lami tangu uhuru

KERO Barabara ya Mbalizi – Iwiji (Mbeya Vijijini) ni kero kubwa, haina lami tangu uhuru

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mimi ni Mwananchi wa Wilaya ya Mbeya Vijijini nina kero ambayo inatutesa sana Wananchi wa Wilaya hii.

Kero kubwa iliyopo kati ya kero zingine ni ubovu wa Barabara ya kutokea Mbalizi hadi Iwiji ambapo inapita Isangati, Santilya, Ilembo, Shigamba hadi Iwiji, kisha inaunganisha Mbeya Vijijini na Ileje.

Tangu uhuru, hii barabara haijawahi kuwekwa kwenye mkakati wa kuweka lami japo kila kipindi cha uchaguzi Wanasiasa wanatuahidi kwamba watahakikisha inakuwa kwenye kiwango cha lami lakini haijawahi kujengwa kwenye kiwango hicho.

Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kupitia CCM, alitoa hoja bungeni 03/02/2026 kwamba ujenzi unaohitajika ni Kilometa 10 na wakati ni zaidi ya Kilometa 30.

Picha hii ni kipande cha barabara maeneo ya Kitongoji cha Italazya


1770400179038.png
 
Back
Top Bottom