Barabara ya Njia 4 Kibaha - Morogoro itakuwa na Tozo

Madini,gesi,utalii kwa viongozi waelevu vinatosha kabisa kuendeshea nchi ila hawa wala keki wa taifa kikubwa wanachofikiria ni kumkwamua mlalahoi ili waendeshe nchi!
Yani nikipewa madaraka nitakuwa Magufuli x 10 yake sicheki na boya. Kazi tu!

Maadui zangu ni wajinga wajinga wezi na mafisadi ndio ntawanyoosha. Hukumu ni shaba tu hamna kingine. Ukikutwa umedokoa hela na ushahidi ukapatikana jua ni shaba moja kwa moja.
 
Napinga kwa nguvu zote huu utaahira, tozo tunazokatwa zitumike kujenga hiyo barabara, kufanya hivi ni sawa na kuiuza nchi vipandevipande na kutuuza wanachi utumwani
 
Aliyejenga njia 8 Ubungo - Kibaha yeye hakuona umuhimu wa tozo au nyie ndio mnaijua sana hela?
Kwa mtanzamo wangu naona Sawa Tu kwasababu serikali hawataingiza pesa zao kwenye mradi kitakachofanyika ni kutangaza tender na atakayeshinda atatengeneza barabara na ikikamilika ataanza kutoza pesa ili hela yake irudi(shida itakuja Kwa huyu mzabuni anaweza kupiga pesa Kwa miaka mingi huku akitoza hela nyingi Kwa gari moja)..
Serikali ingekuwa ina Akili timamu wangetia hela wenyewe Tu
 
Tuko razi kulipia Toll kama tunatumia huduma tutalipa Tozo sio hizi Tozo za Mwigulu ambazo ni za zulma tu.

Napinga kwa nguvu zote huu utaahira, tozo tunazokatwa zitumike kujenga hiyo barabara, kufanya hivi ni sawa na kuiuza nchi vipandevipande na kutuuza wanachi utumwani
Hii ni kama style ya wenye nyumba kariakoo yaani unaingia mkataba na mwenye mpunga Kwa miaka 30 anabadilisha nyumba yako na kuwa ghorofa la biashara na baada ya miaka 30 mjengo unarudi kwako...
Acha tuingie Huko Tu kuliko kusubiri tozo zijenge barabara hii
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba πŸ˜‚ mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Limbukeni, mchunga ng'ombe,poripori.sasa tu niwambie watu wa bush huwa Ni watu wa kazi na hawana shobo na kuwapandishia watanzania gharama za maisha Kama za umeme ama kusaini software kwa 69bilioni yaani kufuatilia umeme ulipokatika nchini.


Watu wa bush huwa Wana Ile feelings ya mtu wa chini. Akifanya maamuzi anamuwaza mama mwenye beseni la ndizi kichwani na mtt mgongoni.
 
Hizi hazijengwi kwa Kodi yetu Basi tusilipe Kodi ili tuwe tunalipia hiyo road sio mbaya.
Mafuta toeni Kodi,sukari,mitumba ,sabuni,mafuta ya kula ,wanataka Vita ipiganwe. Sema huwa naamini hakuna maendeleo bila ya umwagaji wa damu ama sie blacks tuna shida zetu.
Maana hizi Singapore Malaysia China waliwataliwa na hapo miaka ya 60 tulikuwa nao sawa kiuchumi yaani gape Ni negligible mno sema Ni Kama hakuna Ila saivi tunawaomba Msaada. Jitahidi ufanye kizazi chako kiwe cheupe mbona Kama huko Argentina wali whatize waafrika wakaishia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…