Barabara ya Njia 4 Kibaha - Morogoro itakuwa na Tozo

Yani nikipewa madaraka nitakuwa Magufuli x 10 yake sicheki na boya. Kazi tu!

Maadui zangu ni wajinga wajinga wezi na mafisadi ndio ntawanyoosha. Hukumu ni shaba tu hamna kingine. Ukikutwa umedokoa hela na ushahidi ukapatikana jua ni shaba moja kwa moja.
Ahahahahah shaba moja kwa moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kulikoni huyo mzabuni bora serikali ichukue tozo yenyewe. Sababu gharama ya kusafiria barabara kwa hizo kilometre inaweza kuwa ndefu kichizi. Ila bora ilimradi isiwe na matrafiki tu ambao ni kero namba 1
Extrovert,

US kuna barabara mtu kama wewe amejenga, let's say mtu anataka kwenda Airport JK nyerere, kufika JK Nyerere Airport kuna pathways tofauti tofauti.

Katika Pathways za kufika Airport kuna ambazo zina foleni na hazilipiwi- free of charge na zimejengwa na zimekuwa financed za serikali na mara nyingi ni ndefu na time consuming.

Another pathway nyingine unakuta sasa imejengwa na kampuni fulani au na mtu kawa wewe extrovert, hii pathway mara nyingi hainaga foleni, ni very fast, na the shortest one. Ukipita kwenye hii pathway lazima umlipe extrovert.

Kwenye issue ya tozo kwa wenzetu, hailipwi na watu wote. Wanaopenda kuokoa muda na gharama nyingine ndiyo hugharamikia pale wanapopita. Hazinaga mavizuizi yasiyokuwa na sababu.

Hii barabara ya kibaha to chalinze nadhan lazima watajenga expressway ili hili jambo liwe na tija.
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance
Kwa tabia zetu watanzania na wapinzani,hizo barabara zitajengwa, na itakapofikia kipindi Sasa serikali inaanza kuchukua Tozo kwenye hizo barabara hili kurudisha ghalama alizotumia mkandarasi,utasikia wananchi watakuja kuanza kulalama mitandaoni kuwa tozo ziondolewe na blablaa kibao,na wapinzani nao watavalia njuga, na anaweza tokea miaka hiyo Rais mpenda Sifa za kisiasa akaondoa hizo tozo na mkandarasi akapata hasara au serikali,

Japo lengo Ni zuri Sana, kwamba tujenge kwa fedha zetu,japo tujaribu
 
Ndiyo yatakuwa yaleyale ya DART...

Yani hiyo barabara mpaka waje wairudishe ni mpaka pale hiyo barabara ichakae kwanza.

Hawataikabidhi kwa muda kwa visingizio vya hapa na pale hasa "Bado Hatujarudisha Chetu"..

Na hapo tenda ndiyo utakuta kuna mkono wa mkubwa mmoja.

Yani inshort ni kwamba hapa tayari kuna mkubwa kashaichukua hii tenda.

RIP JPM, ULISEMA TUTAKUKUMBUKA KWA MAZURI NA KWELI YANATIMIA.
kazikwe pembeni yake
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Kazikwe pembeni yake nawewe huende peponi mkuu, yaani serikali isifanye Jambo kisa huyo mungu wenu,,kubarini serikali inaongozwa na walio hai sio waliokufa
 
Kwa tabia zetu watanzania na wapinzani,hizo barabara zitajengwa, na itakapofikia kipindi Sasa serikali inaanza kuchukua Tozo kwenye hizo barabara hili kurudisha ghalama alizotumia mkandarasi,utasikia wananchi watakuja kuanza kulalama mitandaoni kuwa tozo ziondolewe na blablaa kibao,na wapinzani nao watavalia njuga, na anaweza tokea miaka hiyo Rais mpenda Sifa za kisiasa akaondoa hizo tozo na mkandarasi akapata hasara au serikali,

Japo lengo Ni zuri Sana, kwamba tujenge kwa fedha zetu,japo tujaribu
Kwenye miradi yoyote mikubwa ya umma, ni lazima public iwe engaged properly lasivyo hakutakuwa na sustainability.

Common understanding ya makundi yote katika jamii ni muhimu sana, na kupitia forum mbalimbali, hizi changamoto ni rahisi kuwa addressed.
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Mhe. Silvester Koka, mmoja wa wabunge makini kabisa. Hii ni product ya Tambaza alikuwa mbele yangu akiwa na Dr. Mwinyi, Dr. Seche, na wengine wengi.
P
 
Vp mkuu unaona hii project itawezekana kweli au Siasa tuu
STANDARD GAUGE Bado inasua sua
BANDARI KAVU KWALA Bado inasuasua
INDUSTRIAL PARK PWANI Hakuna kinachoendelea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barabara yetu, iliyojengwa kwa kodi zetu, anapewa Mwekezaji aipanue halafu atulipishe tozo? Hao wawekezaji kwanini wasijenge mahighway yao wakaweka hizo tozo? Hizi zilizopo ni Interstate roads zetu, haiingii akilini kuwagawia wawekezaji
 
Jo kuna wakati nadhani zinakufyatuka kidogo
Barabara ya zamani Picha ya ndege mpaka kwa Mfipa madaraja yameshaanza kujengwa
Barabara ya Tamko Mapinga kuna shida na mkandarasi anayetajwa kama Mayanga Construction maana hajajenga hata km 5 tangu 2018
Hiyo ya Kibaha Morogoro iko kwenye maandalizi tangu May
Maandalizi gani hayo wakati ndio kwanza tender inatangazwa?
 
Barabara yetu, iliyojengwa kwa kodi zetu, anapewa Mwekezaji aipanue halafu atulipishe tozo? Hao wawekezaji kwanini wasijenge mahighway yao wakaweka hizo tozo? Hizi zilizopo ni Interstate roads zetu, haiingii akilini kuwagawia wawekezaji
Watajenga mpya ndio watatoza hela, ya zamani inabaki vile vile ya bure.
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Hii inatofauti gani na Ule ujenzi wa bandari Bagamoyo? Kweli viongozi wetu mnavhemka na badala ya kuwasaidia wananchi mnawakatisha Tamaa.
Badala ya kupunguza gharama za safari na masherehe ya kukimbiza mwenye na mikutano ya kuunda tume feki! Pesa za ndani zinatosha kujenga kwani mali ghafi nyingi tunazo.
Ardhi ni yetu.
 
Back
Top Bottom