Barabara ya Njia 4 Kibaha - Morogoro itakuwa na Tozo

Hukupata bahati ya kubondwa risasi ndo maana unasema alikuwa na mapungufu ya kibinadamu
Sasa unahangaika na kichaa akikuumiza utashtaki mahakama ipi? Tatizo mlikuwa mnataka muishi na kichaa kikichaa kichaa!
Yule bwana ukifata mambo yako alikuwa haangaiki na wewe.
 
Hivi Tz KWa Sasa ina watu wa ina GANI ndani ya serikali, ? au hata serikali haipo ila tuonacho ni kivulu tu, Yani mpaka tozo kwenye barabara, kwani ni lazima kujenga Iyo barabara ,lengo nini KWa Sasa au nikuuza nchi twambizane tujue, maana Sasa yanafanyika Mambo ambayo hata mkoloni hakutufanyia
We huoni umuhimu wa barabara ya Dar to morogoro kuwa double road? ...Sasa kwa akili km hz maendeleo yatakuja kwel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wahuni katika ubora wao. Najiuliza mwanaume magufuri aliendeshaje nchi bila kusumbua wananchi kwa kutaka kodi zao, yaani miradi lukuki iliendelea na maisha yalikuwa mazuri wananchi walifurahia, inakuwaje kwa hangaya???. Inamaana wakati mzee anaongoza nchi wao walikuwa wamejifungia hawaelewi miujiza ile hadi kaondoka
 
Yani nikipewa madaraka nitakuwa Magufuli x 10 yake sicheki na boya. Kazi tu!

Maadui zangu ni wajinga wajinga wezi na mafisadi ndio ntawanyoosha. Hukumu ni shaba tu hamna kingine. Ukikutwa umedokoa hela na ushahidi ukapatikana jua ni shaba moja kwa moja.
That is why you will never be
 
Mikopo ya ovyo inatumaliza kodi za ndani zinatumila kwa anasa na waliojichukulia nchi
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Sio hiyo tuu hata Igawa-Mbeya-Tunduma nayo itakuwa na tozo..

Kuna barabara kama 4 hivi zinazojengwa kwa utaratibu huo zote zitakuwa ni toll Road..

Hii ni njia nzuri ya kujenga Barabara nyingi kwa wakati mmja.
 
Barabara inajengwaa kwa Tozoo alafu inatozwaa tozooo...[emoji23][emoji23][emoji23]
 
=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).
Hii nchi naona sasa inatafuta kupinduliwa kwa hizi tozo zilizozidi. Tozo za barabarani zilikuwapo. Tukakubaliana kwamba badala ya kutoza tozo za matumizi ya barabara huko huko barabarani, tuziweke kwenye mafuta, kwamba kila unaponunua mafuta diesel au petroli, kuwe na makato ya tozo ya matumizi ya barabara.

Sasa iweje tuna mnatuambia tutatozwa kutumia hii barabara?

Kama imejengwa na kampuni binafsi serikali inapaswa kufanya mpango kuilipa hiyo kampuni kwa kuchukua sehemu ya makato tunayolipia kwenye mafuta, sio kututoza tozo ya kitu kile kile mara mbili.

Na Samia yupo tu, anakubaliana na uonevu huu?
 
Mi naona wachumi wa serikali wakae chini wapige hesabu zao kisha watwambie nini kama nchi inahitaji kukamilisha kwa muda flani.baada ya hapo ipige gharama zake na igawanywe kwa kila raia mwenye uwezo kwamba anatakiwa achangie kiasi kadhaa kwa muda kadhaa awe amemaliza mchango wake!

Hizi habari za leo hiki,kesho tozo ya kile inatuharibia bajeti binafsi!!
 
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).

Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).

Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.

=====================

SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).

Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.

“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.

Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).

Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.

Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.

Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”

Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.

Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.

Chanzo: HABARI LEO
Bado hewa na mwanga wa jua !!!! it is just a matter of time as the trend of events surface
 
Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Hao wanaowaita wazuri, tozo kila sehemu. Ipo siku watatutoza tozo ya haja ndogo na kubwa!
 
Mpaka siku tutakapo kubaliana kwanza sisi watanzania ni wapumbavu na wajinga kisha tuanze kuukataa upumbavu na ujinga ndo tutazifurusha hizi takataka zilizotufikisha hapa
 
Back
Top Bottom