Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ipo ila sijui utekelezaji utaanza lini
Je, Serikali itumie mikopo ya gharama kubwa kujenga au imtafute Sierra one mwenye mtaji na utayari wa kuwekeza kujenga kipande fulani cha barabara kwa makubaliano fulani ya kurudisha pesa yake na faida kupitia tozo bila kuiongezea mzigo serikali na wakati huo kuongeza accessibility?
Binafsi sera nyingi za hii serikali sikubaliani nazo, lakini kwenye hili naona a good step in the right direction.
Changamoto kubwa ninayoiona ni ulafi, wizi, na ubinafsi. KIJANI ni mafisi, na huwa hawana jema.
Ni kweli dictator, mshamba, ni wawili tu nitawakumbuka katika maisha yangu Nyerere kwa high IQ, na mwendazake kuwa wa ajabu kata lugha, maamuzi, uonevu,ubinafsi, matatizo mengi amesababisha kwa muda mfupi!Si mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Nyerere alikuwa very very evil tu kama meko.Ni kweli dictator, mshamba, ni wawili tu nitawakumbuka katika maisha yangu Nyerere kwa high IQ, na mwendazake kuwa wa ajabu kata lugha, maamuzi, uonevu,ubinafsi, matatizo mengi amesababisha kwa muda mfupi!
Hahahaha huku wacha tufanye tunayoweza sisi wenyeweNa kwa kuongeza tu hatuitaji wapuuzi wanaoitwa askari kwenye barabara ambayo tunailipia tozo.
Wakae kwenye vituo vyao kwa adabu na kushughulika na yanayowahusu.
Eeh huku itakuwa utawala tu, 16O-25O kama kawa 😂😂😂Hahahaha huku wacha tufanye tunayoweza sisi wenyewe
Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
Ni vyema tukabakia hapa | ....... wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).Hii misamiati ndiyo hutumika kutupiga
Fanya reference, Jiwe alikuwa mtu wa kwanza kuwaza kujenga mwendo kasi wa kulipia mpaka chalinze kwa PPP, na alikuwa analihubiri daily. Daraja la kigamboni je? Umesahau mambo ya kupiga mbizi?Aliyejenga njia 8 Ubungo - Kibaha yeye hakuona umuhimu wa tozo au nyie ndio mnaijua sana hela?
Hukupata bahati ya kubondwa risasi ndo maana unasema alikuwa na mapungufu ya kibinadamuSi mlisema kwamba jamaa ni mshamba 😂 mara ooh dikteta. Yule mzee alazwe pema peponi mazuri yake ni mengi kuliko udhaifu wa kibinadamu aliokuwa anasimangwa nao.
Hivi Tz KWa Sasa ina watu wa ina GANI ndani ya serikali, ? au hata serikali haipo ila tuonacho ni kivulu tu, Yani mpaka tozo kwenye barabara, kwani ni lazima kujenga Iyo barabara ,lengo nini KWa Sasa au nikuuza nchi twambizane tujue, maana Sasa yanafanyika Mambo ambayo hata mkoloni hakutufanyiaNaibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya amesema TANROADS imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia 4 kutoka Kibaha hadi Morogoro ambayo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F).
Kasekenya alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na Serikali au na Sekta Binafsi (PPP) kwa utaratibu wa Jenga, Endesha, Rudisha (BOT).
Na hivyo Sekta Binafsi itajenga barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 205 kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha hizo kupitia Tozo za Magari.
=====================
SERIKALI kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) imetangaza zabuni ya ujenzi wa barabara ya njia nne kutoka Kibaha – Mlandizi – Chalinze – Morogoro yenye urefu wa kilometa 205.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Godfrey Kasekenya alilieleza bunge jijini Dodoma Jumanne wakati akijibu swali la Mbunge wa Kibaha Mjini, Sylevester Koka (CCM).
Mbunge Koka alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuijenga kwa kiwango cha lami njia nane barabara ya Dar es Salaam hadi Morogoro.
“Barabara hiyo itajengwa kwa utaratibu wa Engineering, Procurement, Construct and Finance (EPC + F),” alisema.
Alisema gharama za ujenzi wake zitatolewa na serikali au na sekta binafsi (PPP) kwa utaratibu wa jenga, endesha, rudisha (BoT).
Katika utaratibu huo, sekta binafsi itajenga barabara hii kwa fedha zake na kuiendesha hadi pale itakaporejesha fedha zake kupitia tozo za magari.
Katika swali la nyongeza, Mbunge Koka alitaka kujua barabara ya Tamko- Mapinga imekuwa ikisuasua kwa muda mrefu na wananchi wa kata za Tangani na Pangani waliopisha ujenzi wa barabara hiyo lini watalipwa fidia.
Pia aliuliza: “Barabara ya zamani ya Dar es Salaam –Morogoro katika eneo la Picha ya Ndege-Mlandizi, imekuwa msaada mkubwa kunapotokea changamoto katika barabara kuu ya ajali magari hupita katika barabara hiyo, je, serikali ipo tayari kurekebisha barabara hiyo ili kuendelea kutumika wakati barabara kuu inapokuwa na changamoto?”
Kasekenya alijibu kwamba ni kweli barabara ya Tamko-Mapinga inasuasua na baadhi ya watu hawakulipwa fidia. Alisema serikali inalifahamu hilo na inalifanyia kazi ili kuhakikisha wananchi wanalipwa na ujenzi wake unakamilika kwa wakati.
Kuhusu barabara ya zamani ya Picha ya Ndege-Mlandizi kufanyiwa maboresho, alisema analichukua hilo kama wizara atazungumza na Tanroads ili kuangalia namna gani wanaweza kuboresha ili kuendelea kuwa msaada wa kukwamua msongamano unapotokea katika barabara kuu.
Chanzo: HABARI LEO