Barabara ya njia nane- Dar - Kibaha yakwama. Serikali yakanusha

Una roho ya korosho zaidi ya shetani,alipoenziwa UN kwa miundombinu aliyotandaza nchini,itakuwa ilikuuma Sana.
 
Miundombinu ya usafri alikuwa anaiweza magufuli tu! Hii wizara ni ngumu sana
Ujenzi ujenzi ujenzi unahitaji akili kubwa tena akili ya kutenda sio siasa
Ni kweli kabisa!! Japo sasa ndio inatoka taarifa ya kukwama kwa ujenzi huo ukweli ni kwamba tangu aondoke JPM duniani, ujenzi wa barabara ulisimama. Kitu pekee kilichoendelea baada ya mzee kuondoka ni ujenzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu pale mbezi karibu na stendi. Kambi kuu ya ujenzi iliyopo pale gogoni unayoiona kwenye post #1 ni kama ilishafungwa maana husikii mashine zikifanya kazi. Wakati wa magufuli mitambo ilikuwa inafanya kazi hapo usiku na mchana!!

Sasa hii mitambo hapo inatafunwa na kutu!! Jibu ni kuwa kodi haikusanywi sasa hivi kama inavyotakiwa!! Wafanyabiashara wanamchukulia mama Poa sana!! Asitegemee kuwa watalipa kodi kwa hiari!! Hiyo elimu, huo ufahamu, huo uzalendo na huo moyo hawana na hawawezi kuwa nao!! Hao ni wa kuwatoza kodi kwa lazima na kwa kuwatoza faini kubwa sana wakikwepa kodi ili waone kukwepa kodi hakulipi bali kunagharimu! Ndivyo alivyofanya JPM!!

Kinyume cha hapo hakuna alipaye kodi kwa fahari ya uzalendo!!
Tuwekeze elimu ya kodi kwa watoto kuanzia shule za msingi darasa la kwanza !
Hela kidogo tulizonazo mabeberu wanatupora kwa nguvu kupitia corona!!
 
Sasa nji
Sasa mkuu njia tatu mpaka Dodoma,wakati wao wanakwepa au kupunguza foleni.
Labda ungelisema mpaka Morogoro.
Kwa Dar,hizo njia nne ni sawa tu. Namuombea Mama apambane tu ikamilike.
 
Utanyooka tu na roho yako ya korosho
Yaani wafuasi wa polepole , bado hamjaamini kama mwendazake sasa hayupo daaa, masikini!mimi toka mwazoni siko naye sasa nitanyooka vipi?wakunyooka ni nyie ambao mlikuwa paradiso, sasa mko jehanamu.
 
Umenena ukweli mtupu
 
Acha kutuita Watanzania milioni 60 ni vilaza katika kusimamia miondombinu, haya ni zaidi ya matusi ya nguoni kwetu sote.
Miundombinu ya usafri alikuwa anaiweza magufuli tu! Hii wizara ni ngumu sana
Ujenzi ujenzi ujenzi unahitaji akili kubwa tena akili ya kutenda sio siasa
 
Bado hazijakusanywa zikajaa kwenye mfuko wa Korosho ili zichukuliwe tena.
Ndipo umeulizwa pesa zimekwenda wapi, mbona unang'atang'ata maneno?.
 
Kwahii Msigwa anapingana na Mtendaji Mkuu? Huu ni upuuzi
 
CHADEMA na Lisu walikuchukulia mke?
 
SIO KWELI!!!

Mradi wa ujenzi wa barabara ya njia nane ya Kimara - Kibaha yenye urefu wa kilometa 19.2 haujakwama kama ilivyochapishwa mtandaoni na kampuni ya habari ya Mwananchi.

UKWELI NI KWAMBA
1. Ujenzi wa mradi huu unakwenda vizuri na umefikia asilimia 94.
2. Malipo kwa makandarasi yanafanyika vizuri na ameshalipwa kwa zaidi ya asilimia 90 (takribani shilingi Bilioni 161)
3. Kwa sasa kinachofanyika ni kukamilisha asilimia chache zilizobaki pamoja kuongeza mahitaji mengine ambayo hayakuwepo kwenye mkataba.
4. Mapipa, uzi na kingo ambazo bado zipo barabarani ni kwa sababu za kiusalama kwa watumiaji wa barabara. Haina maana ujenzi umekwama.

PUUZENI UPOTOSHAJI HUO!
 
Kandarasi haonekani site
 
Tanzania ina wanasiasa wabaya sana kuwahi kutokea hapa duniani; yaani serikali mnataarifiwa uhalisia halafu mnakanusha wakati watu wanaona kwa macho hakuna kinachoendelea Tangu mwezi April 2021?

Ajali zimeongezeka kutokana na sakafu ya barabara kutolingana sambamba na ya zamani huku mapipa na uzio wa waya zikisababisha ajali zinazopelekea vilema hadi vifo lakini serikali inaendelea kukanusha!!!

Kila siku barabara hiyo hapakosi ajali sio chini ya nne kati ya Mbezi Mwisho na Kibamba wakati magari na mitambo karibia inapata kutu bado serikali inakanusha!!!!

Imefika mahali sasa waTanzania wakatae kutishwa na kauli zinazochochea ukosefu wa usalama wa maisha ya wananchi wasio na kosa kuhoji ni kwanini mradi hauendi kama ilivyokuwa mwanzo ambapo hatua kwa hatua walikuwa wanataarifiwa na wanaona kwa macho kinachofanyika kinachoakisi thamani ya pesa ya kodi yao.

*Wananchi wana haki ya kuhoji na msiwatishie tafadhali nchi ni yao na rasirilmali ni za kwao ninyi mmepewa dhamana ya muda tu, sio ya viongozi wa kisiasa; hivyo waheshimu uhuru wa maoni yao
 
Alikunyang'anya shs ngapi?
Hao wanaongea tu huku makalio yanatoa pumzi
Hizo.pesa walizokuwa wananyanganywa ni shilingi ngapai ambazo zilikua haziwaishii wanyanganywaji?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…