Alafu Mhe.Diwani na Mbunge wakija kwenu kuomba kura watawaambia mambo yaliyofanyika kwenye utawala wao ni pamoja na ujenzi wa daraja la Busisi, Ndege zimeongezeka, bwawa la Umeme JNyerere.
Naomba muwaulize kama hayo kwa nafasi zao mliwatuma kuyafanya hayo? Majibu watakayo wapeni yatafakari kama yanakubalika basi muwaongezee mitano tena.
Ifike mahali kila Kiongozi apimwe kwa nafasi yake, tusikubali wengine kubebwa na miradi mikubwa ya Kitaifa wakati Mitaani na vijijini kwetu hali siyo nzuri.