KERO Barabara za Ludewa zimesahaulika sana, mvua kidogo tu tayari hazipitiki na leo magari yamekwama huko

KERO Barabara za Ludewa zimesahaulika sana, mvua kidogo tu tayari hazipitiki na leo magari yamekwama huko

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
433
Wakazi wa Luponde halmashauri ya mji wa Njombe na watumiaji wa barabara ya Njombe - Ludewa wameiomba serikali kufanya marekebisho ya muda mrefu ili kuondoa adha ya magari kukwama wakati wa kipindi hiki cha mvua.

Wito huo umetolewa na baadhi ya wakazi wa Luponde akiwemo Colbina Mligo ambapo wanasema changamoto ya magari kukwama haijaanza sasa lakini hali inazidi kuwa mbaya kutokana na mkandarasi aliyekuwa akijenga barabara hiyo kwa kiwango cha zege kusimama muda mrefu na kuacha ikiwa imechimbwa.



Wakati wakitoa wito huo kwa mamlaka kumeshuhudiwa zaidi ya Magari 30 yanayosafirisha mizigo na abiria kupitia barabara hiyo kutoka Wilayani Ludewa kuelekea mjini Njombe kukwama kwenye maeneo tofauti ikiwemo katika eneo la mlima wa Mahove uliopo Luponde kutokana na Changamoto ya ubovu wa barabara.

Nao baadhi ya madereva akiwemo Adam Mwalukovo pamoja Michael Chawe wameiomba serikali kukabiliana na changamoto hiyo ili waweze kufikisha mizigo ambayo mingi ni ya kuharibika.

"Hii barabara ina changamoto kubwa sana na serikali wameshaiona,na mimi niko hapa toka jana saa tisa lakini kama mnavyoona magari hayaendi"amesema Adam Mwalukovo

Hata hivyo licha ya changamoto hiyo tayari serikali kwa kushirikiana na Wakala ya Barabara Tanzania TANROAD mkoa wa Njombe imefikisha Mtambo unaosaidia kuvuta magari yanayokwama.

Jambo TV inaendelea kufuatilia zaidi ili kujua mpango wa muda mrefu wa kuimarisha usafirishaji kupitia barabara hiyo wakati serikali ikiendelea na mpango wa kudumu wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha zege.
 
9 december wajitokeze kwa wingi kwenye maandamani. Rolle royce moja alilonunua abdul kwa kodi zao, gharama yake inatosha kumaliza ilo tatizo likabaki historia
 
Kuna maeneo mengi ambayo yana barabara zisizopitika hasa kipindi cha mvuaa. Na kwa sasa viongozi wanapaswa kuweka jicho zaidi ili kuondokana na adha za usafiri kwa magari na hata watembea kwa miguu
 
Back
Top Bottom