Barabara za mitaani ndani ya Manispaa ya Morogoro zimeharibika hadi kero. Ndugu zetu wahusika, yaani TARURA, wanavuta mpunga tu na kuotesha vitambi bila kujali wakazi wa Manispaa hi pendwa wanateseka kwa barabara zetu kukosa matengenezo.
Ubovu wa barabara hizi ni wa muda mrefu, yapata miaka mitatu sasa, lakini hakuna lolote lililofanyika kutuondolewa adha hii tuipatayo sisi waadhirika. Au mnataka tuandamane kama ndugu zetu wa Kenya?