Barabara za Mji wa Serikali Dodoma zimeshafungwa taa za barabarani

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Huu mji ni moja ya vitu vya kuvutia sana hapa Dodoma. Japo haujakamilika, ila kukamilika kwa mtandao wa barabara tu, teyari kunafanya huu mji upendeze na utapendeza zaidi pale majengo ya magorofa yatapokamilika na mazingira kuboreshwa(kupanda miti, n.k)

Leo nimepita katika huu mji na kukuta teyari taa za barabarani zimefungwa na teyari zinafanya kazi. Hakika kunavutia japo magari bado ni machache.

Ukiacha kukosa utu na makandokando mengine, mji juu ni urithi mzuri aliotuachia Mwendazake na tumshukuru Mama kwa kuendeleza.

Mji huu nimeupenda sana na ninapanga kununua kiwanja na kujenga maeneo ya jirani na huu mji.

Hongera kwa wote waliohusika katika ku- design huu mji ambao ukikakamilka kama ulivyopangwa, basi eneo hili litakuwa kivutia kizuri kwa watanzania na wageni.

A very nice city!
 
Picha iko wapi?
 
Kasi ya ujenzi wa huo mji imepungua sana.Kuna magorofa zaidi ya 50 ambayo ni ofisi za mawizara,ajabu ni kwamba mengi yametelekezwa bila kuisha,yale yanayoendele kujengwa unakuta mafundi ni wachache sana,gorofa linajengwa na mafundi watano peke yake,.
 
Ni sahihi huo mji wa Mwendazake utapendeza ukikamilika, nimewahi kuutembelea mwaka huu ukiwa kwenye hiyo hatua ya Ujenzi.

Hivi Ikulu imefichwa wapi kwenye huo mji? nahisi imetengwa mbali na eneo la Wizara
 
Ikulu haipo, ila kwenye plan, kulikuwa na eneo kwa ajili ya ujenzi Bunge ingawa kwa sasa sijui kama hiyo plan bado iko hivyo.
 
Back
Top Bottom